ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU MAITI 7 ZA MTO RUVU NA KUPOTEA KWA BEN SANANE - See more at: http://www.bongohotz.com/2016/12/taarifa-ya-jeshi-la-polisi-kuhusu-maiti.html#sthash.ULSjwiDp.dpuf

Wednesday, December 21, 2016

post-feature-image

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa ufafanuzi kuhusu miili 7 ya watu iliyokutwa ikielea katika mto Ruvu na kusema kuwa linaendelea na upelelezi kwa lengo la kuwatambua marehemu hao. Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa
Upelelezi wa makosa ya Jinai Kamishna wa Polisi Robert Boaz, amesema jeshi hilo bado halijawatambua marehemu hao, huku akitetea uamuzi wa jeshi hilo kuzika haraka miili ya marehemu 6 kati ya 7. “Hatua zote za kitaalam zilifuatwa na tunaendelea kufanya upelelezi unaolenga kuwatambua marehemu hao na kujua ni jambo gani liliwasibu, tunawasihi wananchi kuendelea kutupa taarifa zitakazosaidia kutambulika kwa marehemu hao” Amesema Boaz Akielezea jinsi jeshi hilo lilivyopata taarifa, amesema jeshi hilo lilipata taarifa za kuelea kwa maiti 7 katika mto Ruvu eneo la Mkuruge wilayani Bagamoyo kati ya tarehe 6/12/2016 hadi 9/12/2016 ambapo askari na daktari walifika katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa kitaalam. Amesema miili 6 kati ya 7 ilikuwa imeharibika sana na ndiyo maana iliamuliwa zizikwe katika eneo la tukio wakati moja yenye unafuu ikipelekwa hospitali ya wilaya ya Bagamoyo hadi tarehe 16/12/2016 ilipozikwa na halmashauri baada ya kutotambuliwa na tu yoyote. Kuhusu kutoweka kwa msaidizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Ben Sanane, Kamishna Boaz amesema jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kubaini mahali alipo na kilichomsibu. Hii ni sehemu ya taarifa yake. - See more at: http://www.bongohotz.com/2016/12/taarifa-ya-jeshi-la-polisi-kuhusu-maiti.html#sthash.ULSjwiDp.dpuf

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU