Mkuu wa mkoa wa njombea Christopher Olesendeka ameuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya wangingo’mbe ikiwemo ofisi ya mkurugenzi kuhakikisha inamchukulia hatua za kisheria mtumishi wa idara ya fedha Edward kigoda kufuatia ubadhirifu wa fedha zaidi ya shilingi milioni 37 ambazo alikiri kuzichukua kinyemela na ameanza kurejesha
Akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa ofisi za utawala na nyumba za watumishi Wilayani humo mkuu wa mkoa amemtaka Kaimu meneja wa wakala wa majengo wa mkoa wa njombe TBA Baziri mwakilao kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya hiyo haraka ambayo ujenzi wake umeanza kuingia dosari
Halmashauri ya wilaya ya wangingombe ilianzishwa mwaka 2012 imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa ofisi za mkurugenzi kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 697 ingawa halmashauri hiyo ingali inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa vyombo vya usafiri.
No comments:
Post a Comment