ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Mabomu 3 yalipuka adhuhuri Bujumbura

Wednesday, February 3, 2016



Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa vibaya katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura
Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa vibaya katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kufuatia milipuko 3 ya gruneti.
Duru zinasema kuwa takribana watu wanne wamejeruhiwa baada ya watu wasiojulikana kutupa gruneti nje ya jumba la posta mjini Bujumbura.
Mlipuko mwengine ulitokea nje ya afisi za kampuni inayotoa huduma za simu nchini humo Lumitel.
Mlipuko wa tatu ulisikika takriban nusu saa baadaye katika soko la zamani.
Hadi tulipochapisha taarifa hii hakuna maelezo kamili hayajatolewa kuhusu nani aliyetekeleza mashambulizi hayo na kwanini.
Machafuko nchini humo yalitibuka mwezi Aprili mwaka wa 2015 baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania uchaguzi katika muhula wake wa tatu.
Wapinzani wake walisema Nkurunziza alikuwa anakiuka katiba ya taifa na kisha maandamano yakaanza kukotokea.
Kulitokea jaribio la mapinduzi ambayo ilizimwa na kisha rais huyo akaibuka mshindi katika uchaguzi ambao ulisusiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa upinzani.
Machafuko nchini humo yalitibuka mwezi Aprili mwaka wa 2015 baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania uchaguzi katika muhula wake wa tatu.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Prime Ndikumagenge, anasema kuwa mashambulizi haya leo ni ya kipekee kwa sababu ni mara ya kwanza kuwahi kutokea mchana.
''kumekuwa na mashambulizi mengi nchini ,lakini hii ndio mara ya kwanza kwa mashambulizi ya aina hii kutokea mchana''.
Takriban watu 439 wameuawa huku wengine 240,000 wakitoroka nchini kuwa wakimbizi nje ya nchi kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.
Mwezi uliopita shirika linalopigania haki za kibinadamu Amnesty International walisema kuwa picha za setlaiti zinaonesha uwezekano wa kuweko kwa makaburi 5 ya halaiki nje ya Bujumbura.
Maafisa wa usalama wanalaumiwa kwa kuua watu mwezi desemba mwaka uliopita.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU