Ligi kuu Tanzania bara kuendelea leo tena , wapenzi na wanachama wa Yanga hisia zetu zote na dua tutazielekeza uwanja wa Sokoine jijini Mbeya!Ambapo Yanga itakuwa na mtihani wa kusaka pointi 3 ugenini dhidi ya Tanzania Prisons.
Mara nyingi Tz Prison imekuwa haipati matokeo mazuri mbele ya Yanga, licha ya hivyo Mchezo wa leo unategemewa kuwa mgumu wenye ushindani hasa kutokana na ubora wa sasa vilabu hivyo.Tanzania Prison ipo nafasi ya 7 kwa alama zake 27 baada ya kucheza michezo 15,imeshinda michezo 3 sare 1 na kufungwa mchezo 1 katika michezo yake 5 ya hivi karibuni,Kwa upande wa Yanga wapo nafasi ya 1 katika michezo 16 wamekusanya alama 39 huku wakipoteza mchezo 1 tu na kushinda michezo 4 katika jumla ya michezo yao 5 ya mwisho.
Mchezo wa leo una maana kubwa kwa timu zote mbili lakini Yanga ndio zaidi, lazima watacheza kwa juhudi ili wapate ushindi kwanza ambao utashusha presha ya mashabiki ambao walifedheheshwa na kipigo cha goli 2 - 0 kutoka kwa Coastal Union,matokeo yoyote yasiyo ushindi basi yatapokelewa kwa hisia tofauti!Pili ushindi huo utaamsha ari ya ubingwa na kuendelea kuwakimbia watani Simba ambao wanahaha kufuta pengo la pointi 3_____ Matokeo mbali na ushindi leo ina maana ubingwa utakuwa umewekwa rehani hasa ukizingatiwa Azam watakuwa na michezo 2 mkononi.
Kuendelea kucheza mchezo ule ule, kikosi kile kile ,mbinu zile zile kama timu ipo uwanja wa Taifa inaweza kuwagharimu Yanga.Tayari vilabu vingi vishaujua udhaifu wa Yanga hasa ikiwa mikoani , huku kocha wa Coastal Union akijinasibu kuwa unapaswa kujaza viungo wengi pia hakikisha unampiga pin Thaban Kamusoko ambaye ndiye injini ya Yanga sehemu ya kiungo!bila shaka kocha wa Prison alikuwa na muda mzuri kufuatilia mchezo huo ili kujua udhaifu wa Yanga upo wapi _____ Ni mtihani kwa Mdachi Hans Van Pluijm ambaye atalazimika kuja kivingine na inawezekana akaongeza idadi ya viungo badala ya viungo wawili.
Jeremiah Juma ndiye mchezaji wa kuchungwa zaidi kwa wachezaji wa Prisons,mshambuliaji huyu ana magoli 9 tayari!Yanga wao wanategemea kumpokea kiungo wao Haruna Niyonzima huku Deus Kaseke , Donald Ngoma na Paul Nonga wakihofiwa zaidi na wajela jela hao.
Michezo 3 Ya Mwisho.
___Feb 23, 2015 (Ligi kuu / Sokoine Stadium)
Tz Prisons 0 - Yanga 3.
___Aug 12 , 2015 (Kirafiki / Sokoine Stadium )
Tz Prisons 0 - Yanga 2.
___ Sept 16 , 2015 (Ligi kuu / U.Taifa)
Yanga 3 - Tz Prison 0.
Maoni ya Hans Van Pluijm.
“Mpira ni jambo lenye mambo mengi, sisi hatujawahi kucheza tukitaka kupoteza. Imetokea tumepoteza, si jambo zuri kwa mtu mwenye malengo ya kutwaa ubingwa.
“Mpira ni jambo lenye mambo mengi, sisi hatujawahi kucheza tukitaka kupoteza. Imetokea tumepoteza, si jambo zuri kwa mtu mwenye malengo ya kutwaa ubingwa.
“Lakini tutapambana, tutaendelea kurekebisha mambo ili kwenda vizuri kwa hatua nyingine,” alisema Pluijm.
Tujitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu, ushindi wa leo ni muhimu sana katika mbio za ubingwa!Shime Wananchi tukaijaze Sokoine leo.
No comments:
Post a Comment