ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

MAMBO HAYA 10 YANAWEZA KUOKOA MAHUSIANO AU NDOA YAKO!

Saturday, February 27, 2016

Mapenzi.Mahusiano,Ndoa,Maisha

Mahusiano sio jambo rahisi. Haishangazi kuona kwamba eneo la mahusiano ya binadamu, iwe ni kwenye ndoa,mapenzi,kazi,biashara na jamii ni mojawapo ya eneo linalopewa kipaumbele cha kila aina. Wataalamu wa saikolojia kila siku wanakesha wakijaribu kugundua mbinu mpya za kuboresha mahusiano ya binadamu.

Pamoja na “ugumu” wa mahusiano ya kibinadamu, yapo mambo kadhaa ambayo yanakubalika miongoni mwa wengi wetu kwamba yakifanyika kwa uwazi,upendo na bila hila, yanaweza kusaidia sana katika kuboresha mahusiano hayo. Haya hapa ni mambo 10 ambayo yanaweza sio tu kuboresha bali hata kuokoa mahusiano yako hususani mahusiano ya kimapenzi au ndoa.


  1. Kuomba Msamaha (Samahani)- hakuna binadamu aliye kamili. Sote tuna mapungufu. Mapungufu hayo huja au kuwa dhahiri kwenye mahusiano na hata kwenye ndoa. Kuna kukosea. Kuna kumkosea mwenzako. Na mara nyingine unaweza kukosea kwa bahati mbaya tu bila kukusudia. Ukigundua kwamba mwenzako hajafurahishwa na ulichofanya au kutofanya, omba msamaha. Hata kama huelewi kwa undani kwanini mwenzako kakasirika au hata kama wewe unaona ni jambo dogo tu, omba msamaha.

  1. Tumia Neno Tafadhali- Unapoomba kufanyiwa au kusaidiwa kitu, tumia neno tafadhali au naomba. Badala ya kusema Baba Nanihii,niletee maji ya kunywa,sema, “Baba nanihii tafadhali naomba niletee maji ya kunywa”. Ni maneno madogo tu lakini yanatosha kuonyesha heshima na upendo kwa mwenzako.

  1. Sema Asante(Shukuru)- Kila unapopewa kitu, kufanyiwa jambo,kusifiwa nk onyesha upendo wako kwa kusema “Asante”. Usiposema asante usishangae siku nyingine usipopewa au kufanyiwa kitu fulani.

  1. Mwambie mwenzako Unampenda- Anajua kwamba unampenda na pengine ndio maana yupo na wewe. Lakini hakikisha unamkumbusha. Usimchukulie poa tu. Hapana. Haya mwambie mwenzako unampenda sasa hivi.

  1. Samehe na Sahau- Kama nilivyosema hapo juu, binadamu hatupo kamili. Tunakosea. Mara nyingine tunakosea kila mara na kwa jambo lile lile. Jifunze kusamehe na kusahau. Usisamehe kwa minajili ya kuzuga amani ili ulipize kisasi. Samehe na sahau. Usikumbushe yaliyopita. Jifunze kutokana na yaliyopita ila samehe na muombe Mungu usahau.

  1. Ongea Lugha Ya Umoja Badala ya Umimi- Binadamu tu-wabinafsi. Ni hulka. Tunajiangalia sisi kwanza kabla ya kumwangalia mtu mwingine hata akiwa mpenzi, mume au mke. Lakini ukitaka mahusiano yadumu, ni muhimu kubadili “lugha”. Badala ya kuongelea mambo katika umimi, ongea katika wingi(sisi). Kwa mfano badala ya kusema,’ nyumba yangu au gari langu”(hususani kwa walio kwenye mahusiano ya ndoa) sema, “nyumba yetu na gari letu”. Hutopungukiwa kitu ila utaijaza akaunti yako ya mahusiano mema.

  1. Muite kwa Jina Lake- Ushakwenda mahali kama benki vile ukasoma jina la mhudumu aliyepo mbele yako kupitia kitambulisho chake kisha ukamuita kwa jina? Uliona jinsi alivyokupa huduma nzuri zaidi? Binadamu (hususani wanaume) tunapenda kusikia majina yetu yakitajwa. Ni hulka. Hakikisha unamuita mwenzako kwa jina lake. Litumie katika mazungumzo ya kila siku na kila mara.

  1. Sikiliza- Kuna nyakati mpenzi wako anachotaka ni sikio lako tu. Sikiliza kwa makini anachokuambia. Onyesha wazi kwamba unasikiliza. Epuka na tabia ya “kumsikiliza” mwenzako huku unachezea simu yako au unakodolea macho televisheni.

  1. Mheshimu- Hili linaonekana kuwa la wazi, si ndio? Kwa bahati mbaya mahusiano mengi yanavunjika huku wanaoachana wakisema “kutoheshimiwa” ndio sababu kubwa ya wao kuamua kujitoa. Kila mtu ana jinsi yake ya kuona anaheshimiwa au kudhauraliwa. Kwa makini jaribu kujua mambo yanayomfanya mwenzako aone umemdharau au kutomheshimu. Ikiwezakana muulize. Msome. Kisha yaepuke kama ukoma.

  1. Msaidie Mwenzako- Ni muhimu sana kusaidiana. Hata pale ambapo mwenzako hajaomba msaada, fikiria kama Ingekuwa wewe ungehitaji msaada? Kama ni ndio, basi msaidie. Kwa mfano, msaidie kupika, kufua, kusafisha gari, kununua mahitaji ya Nyumbani, kusafisha nyumba, kuvalisha watoto. Kila inapowezekana (na mara nyingi inawezekana) msaidie.


Jisikie huru kuongeza hapa chini mambo mengine ambayo unaona ni muhimu na yanaweza kuokoa mahusiano.

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro Lakamata Bunduki Ikiwa Imefichwa Kwenye Tundu la Choo.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Ramadhan Mungi akionesha Bunduki aoina ya Short Gun iliyokamatwa ikiwa imefichwa katika tundu la Choo katika eneo la Shirimatunda katika manispaa ya Moshi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Ramadhani Mungi akizungumza na wanahabari kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika mkoa wa Kilimanjaro hivi karibuni.


Na.Dixon.Busagaga,wa Globuu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wa watatu kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbalimbali likiwemo la mauaji pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.
Mbali na watuhumiwa hao Polisi pia imefanikiwa kukamata Bunduki aina ya shortgun (Pump Action) yenye namba 69901 ikiwa imefichwa katika tundu la choo nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa hao  eneo la Shirimatunda  katika manispaa ya Moshi.
Bunduki hiyo pamoja na risasi tatu imetajwa kukodishwa na watuhumiwa na kisha kutumika katika shughuli za kihalifu ikiwemo uporaji wa fedha katika maeneo tofauti na mali huku ikihusishwa pia kufanya mauaji.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishina msaidizi wa Polisi, Ramadhani Mungi alithibitisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na bunduki na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika.
“Katika siku za mwisho wa Desemba mwaka jana na siku za mwanzoni za mwaka huu ,kulikuwa na wimbi la matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya Short gun ambayo pia ilisababisha mauaji,tayari tumewakamata watu kadhaa na jana (juzi) asubuhi tuliweza kuikama silaha aina ya Short gun.”alisema Mungi.
Wakati huo huo matukio ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto yameendelea kushika kasi mkoani ambapo hivi karibuni mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa ) alikatwa matiti yote mawili baada ya kujinasua katika jaribio la kubakwa.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa,Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo kuwa ni Anold Josephate ambaye alitoweka na matiti hayo baada ya kuyaweka katika mfuko wa plastiki.
Alisema tukio jingine linalo ashiria kuongezeka kwa makosa ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ni tukio la juzi ambapo mwanamke mmoja aliyfahamika kwa jina la Vailet Apiniel ameuawa baada ya kunyongwa shingo.
“Siku za karibuni hapa yamejitokeza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yanayo uaibisha mkoa wetu,matukio ya ubakaji,matukio ya watu kutupa vitoto,haa ni matukio mabaya na jana tu kuna mwanaume aitwaye Denis Shayo alimnyonga mke wake”alisema Mungi.
Alisema eneo hili linahitaji kutolewa elimu ya kutosha huku akizitaka taasisi zinazojishughulisha na utetezi wa masuala ya kijinsia kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na matukio kama hayo .

Waziri Mkuu Asubiriwa Kwa Mabango Kiteto


Wananchi  wilayani Kiteto  mkoani  Manyara  wamejiandaa  kumpokea  kwa  mabango  Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  ili  kutoa  ujumbe  wa  kuwakataa  baadhi  ya  viongozi  wa wilaya  kutokana  na   kukithiri  kwa  migogoro  ya  ardhi.

Miongoni  mwa  viongozi  wanaotajwa kuwamo  katika  ujumbe  huo  ni  Mkuu  wa  Wilaya Kanali Samweli Nzoka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bosco Ndunguru,Katibu Tawala (DAS) Nicodemus John pamoja  na  kamanda  wa  Polisi  wa  Wilaya (OCD) George Katabazi.

Hata  hivyo DC Nzoka  amepiga  marufuku  mwananchi  yeyote  kuandaa  bango  lolote  katika  ziara  hiyo  ya  Waziri  Mkuu  inayotarajiwa  kufanyika  Februari  29  mwaka  huu.

Akizungumza katika kikao  cha  baraza la  Madiwani  jana,Nzoka  alisema  hataruhusu  kuandaliwa  wala kuonyeshwa  mabango  hayo  kwani  ni  ishara  ya  vurugu  na  uvunjifu  wa  amani.

Mkuu  huyo  wa  Wilaya  alisema  anazo  taarifa  za kuwapo  watu  walioandaliwa  kutoka  wilaya  na  mikoa  ya  jirani  kwenda  Kiteto  kuzomea baadhi  ya  viongozi  wa  Wilaya katika  ziara  hiyo.

Katika  ziara  hiyo, Majaliwa  atakutana  na  kuzungumza  na  viongozi  mbalimbali  wakiwemo  madiwani, wakuu  wa  idara  na  viongozi  wa  mila  wa  jamii  ya  wafugaji

Waziri  mkuu  anategemewa  kutoa suluhisho  la mgogoro  wa  ardhi  kati  ya  wakulima  na  wafugaji  uliodumu  kwa  muda mrefu  na kusababisha  mauaji

KANISA LACHOMWA MOTO SHINYANGA BAADA YA VIONGOZI WA KANISA KUTUMBULIWA JIPU

Thursday, February 25, 2016



Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Mika Nyange 

Kanisa la True Jesus lililopo katika  kijiji cha Igalamya kata ya Usule tarafa ya Samuye wilaya ya Shinyanga limechomwa moto na watu wasiojulikana kutokana na kile kinachodaiwa kuwa baadhi ya viongozi kanisa hilo walitumbuliwa jipu kwa kusimamishwa kuhudumu katika kanisa hilo.
 Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Mika Nyange  kwa vyomba vu ahabari tukio hilo limetokea Februari 22 mwaka huu saa sita usiku. 

Kamanda Nyange amesema chanzo cha tukio hilo ni baadhi ya viongozi wa kanisa hilo lililoezekwa kwa nyasi kusimamishwa kuhudumu katika kanisa hilo kutokana na kuwakaribisha wageni kutoka Kenya katika kanisa hilo bila kufuata utaratibu. 


Akifafanua zaidi Kamanda Nyange amesema kwa mujibu wa Askofu wa kanisa hilo Albinus Kichele viongozi waliosimamishwa kuhudumu katika kanisa hilo ni mwinjilisti wa kanisa Yona Nkuba na wainjilisti na walimu wa kanisa ambao ni John Peter,Jackson Bundala na Thereza Salamba. 
 Amesema kutokana na wageni hao kuingia bila kufuata utaratibu wa kanisa wageni hao walikamatwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Shinyanga kisha kurudishwa kwao Kenya hali iliyosababisha viongozi hao wa kanisa kujitoa kwenye kanisa hilo kabla hawajasimamishwa. 

Kamanda Nyangi alisema jeshi la polisi mkoani Shinyanga linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo. 

BAADA YA MAJIPU KIBAO KUTUMBULIWA KAMERA 486 ZAFUNGWA BANDARI YA DAR ES SALAAM



Zikiwa zimepita siku chache tangu waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam na kubaini uozo wa kuchepushwa kwa bomba la mafuta mamlaka hiyo imekuja na mpango madhubuti wa kuimarisha usalama katika bandari hiyo kwa kufunga mfumo mpya wa kamera 486 zenye uwezo wa kuonyesha matukio yote yanayotokea nje na ndani ya bandari hiyo na hasa katika eneo la kupakulia mafuta. 
 
 
ITV ilifika bandarini hapo na kushuhudia namna kamera hizo zinavyofanya kazi huku afisa mlinzi mwandamizi Bw Kiswiza Lukasi akielezea namna mashine hizo zinavyofanya kazi.
 

Naye Bi Janeth Ruzangi meneja mawasilino wa TPA amesema mashine hizo zinaonganisha na banadari zote lengo ni kuakikisha kuwa usalama unaimarika katika bandari za hapa nchini. 
 

Baadhi ya watumiaji wa bandari hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia utendaji na usalama wa bandari hiyo lakini kwa sasa wanapata imani kuwa mali zao zitakuwa salama.

MAGUFULI AWALAZA NJAA WAPIGA DILI TANZANIA


Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, imeamua kutumia mfumo wa ‘Cash Budget (kutumia kilichokusanywa), huku baadhi ya wachumi wakisema utaleta nidhamu ya matumizi ya serikali na kubana watumishi ambao walizoea kutumia vibaya fedha za umma kwa kuzipangia matumizi yasiyo na tija. 

Wizara ya Fedha na Mipango imeieleza Nipashe jana kuwa, mfumo wa kupanga na kutumia kinachokusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA), ndiyo ulioamuliwa kutumiwa na serikali ya awamu ya tano. 

Itakumbukwa kuwa, tangu Novemba mwaka jana, mapato ya TRA yalipanda kutoka wastani wa Sh. bilioni 800 na Sh. bilioni 900 kwa mwezi mpaka Sh. trilioni 1.3, Desemba, mwaka jana Sh. trilioni 1.4, Januari, mwaka huu Sh. trilioni 1.06 na malengo ya Februari ni kukusanya Sh. 1.03. 

Jana Ofisa Habari wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ingiaheddi Mduma, alisema utaratibu wa kutumia kilichokusanywa utaendelea kutumika kila mwezi. 

Alisema kila makusanyo yatakayopatikana kwa mwezi husika, yatatumika kulingana na mahitaji husika ya mwezi huo. 

“ Mahitaji yakiwa mengi katika mwezi husika, basi hata fedha itakayokusanywa kwa mwezi huo itatumika kulingana na mahitaji hayo, tutakuwa tunafanya hivyo kila mwezi,” alisema Mduma. 

WASOMI WAZUNGUMZA 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Wilhelm Ngasamiaku, alisema mfumo ambao unatumiwa na serikali ya awamu ya tano unajulikana zaidi kama ‘Cash Budget,’ ambapo mipango na matumizi ya serikali inabidi ipangwe kutokana na kile 
kinachokusanywa. 

“Kutumia kile unachokipata hiyo ndiyo ‘Cash Budget’, siyo mara ya kwanza mfumo huu kutumiwa hapa nchini hata miezi ya mwisho ya serikali ya awamu ya nne baada ya wahisani kuacha kutoa misaada, ulitumika. 

Huu mfumo faida yake unaleta nidhamu ya matumizi ya serikali kwa hiyo inaifanya itumie na kupanga kutokana na makusanyo yake ya ndani, ndiyo sifa pekee ya mfumo huo. 

“Hasara yake ni kwamba unaposhindwa kukusanya mapato ya kutosha, matumizi yako mengi uliyopanga kuyafanya utashindwa kuyagharimia na kwa sababu unatumia unachokusanya ni lazima nguvu nyingi zielekezwe kwenye kukusanya,” alisema Dk. Ngasamiaku. 

Alisema kwa muda mfupi ambao Rais Magufuli ameanza uongozi wake, suala la makusanyo limeongezeka kuanzia Novemba, Desemba na Januari, ingawa fedha za nyuma ambazo hazikukusanywa zimesaidia ongezeko hilo. 

Alisema kuongeza zaidi mapato kutawezekana endapo biashara nyingi za wajasiariamali wadogo na wa kati zitatozwa kodi, jambo ambalo sasa hivi halifanywi kwa ufasaha. 

Kuhusu matumizi kadhaa aliyofayanya ikiwa ni pamoja na kukata fedha za sherehe za uhuru na za wabunge, alisema hatua hiyo ilichukuliwa kwa kuwa aliingia madarakani bajeti ya mwaka 2015/16 ikiwa imeshapita. 

“Ikumbukwe alipoingia madarakani bajeti ilishasomwa, kwa hiyo hivi vitu ambavyo siyo lazima kama hizo sherehe za uhuru, za wabunge, semina elekezi fedha zilikuwa zimeshatengwa kwa shughuli hiyo, akaona ni vyema kupeleka kwenye masuala muhimu zaidi,” alisema na kuongeza: 

“Hiyo ilikuwa ni re-allocation tu ya kawaida na kwa sababu makusanyo ni makubwa anayatumia kutekeleza baadhi ya ahadi zake ambazo hazikuwa kwenye bajeti,” alisema. 

Mhadhiri wa UDSM na mtaalam wa uchumi, Dk. Haji Semboja, alisema anachofanya Rais Magufuli sasa kiliwahi kufanywa na marais waliomtangulia.

Alisema tofauti yake na marais hao ni kuwa, Rais Magufuli anatumia kutokana na kile alichokikusanya, tofauti na watangulizi wake waliokuwa wanatumia kutoka katika kile walichokopa. 

“Unashona nguo kulingana na ukubwa wa kitambaa chako, mfumo huu ni mzuri kwa kuwa anatumia kutoka kile alichokusanya na nchi haitakuwa na deni kubwa miaka ya mbele,” alisema. 

Dk. Semboja alisema mfumo wa kutumia fedha katika sekta mbalimbali ni mzuri kwa sababu, mtu anatakiwa kutumia kulingana na kile alichonacho na siyo asichonacho. 

Naye Mkuu wa Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Jehovaness Aikaeli, alisema ni utaratibu mzuri ulionzishwa kwa kuwa unasaidia kuziba mashimo yaliyokuwapo tangu awali. 

Alisema haina haja kwa serikali kuweka akiba wakati wananchi bado wanahitaji kupata mahitaji muhimu kama vile dawa hospitalini na madawati katika shule. 

“Haina haja ya kuweka akiba, kama vile alivyofanya fedha za sherehe za uhuru zielekezwe katika ujenzi wa barabara ni sahihi, utaratibu huu uendelee na usiishie njiani,” alisema. 

Dk. Aikaeli alisema katika nchi yoyote duniani kanuni kubwa ni kutegemea kodi katika kuendeshea nchi, hivyo Rais Magufuli anatakiwa kuendelea kuziba mianya ya upotevu wa kodi. 

Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha Dar es Salaam, Dk. Bill Kiwia, alisema ni mfumo mzuri aliouanzisha Rais John Magufuli katika kuinua uchumi wa nchi. 

Hata hivyo, alisema serikali inapaswa kutotegemea makusanyo ya kodi pekee katika bajeti yake, bali iangalie vyanzo vingine vya mapato, kwani kwa kutokufanya hivyo kutaua sekta binafsi. 

Alisema serikali pia inapaswa kuangalia makusanyo katika vitalu vya madini na gesi, ushuru na tozo. 

Alisema pia serikali inaweza kutumia njia ya kukopa fedha kutoka mataifa ya nje na kuzielekeza katika sekta za maendeleo. 

“Serikali isitegemee sana makusanyo ya kodi katika kutekelezea bajeti yake, inaweza kuangalia vyanzo vingine vya mapato, lakini ni mfumo mzuri aliouanzisha Rais, utasaidia kukuza uchumi wa nchi,” alisema Dk. Kiwia. 

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia (WB) ya Julai, 2015, uwiano wa wigo wa kodi ni asilimia 12. 

Alisema Tanzania inahitaji kukusanya kodi zaidi ili iweze kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji serikali na kwamba kupungua kwa misaada na vikwazo katika mikopo ndio kunapelekea umuhimu wa kukusanya kodi zaidi.

Alisemal akini ni muhimu ukusanyaji huo wa kodi usidhoofishe sekta binafsi. 

Akizungumzia operesheni ya kukusanya kodi inayoendeshwa na TRA, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo, alisema lengo lake ni kusajili wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa na kukagua ambao wanapaswa kutumia mashine za EFDs lakini hawazitumii. 

Alisema operesheni hiyo ni ya kawaida na inafanyika nchi nzima na kuwa wale ambao watakutwa wanafanyabiashara bila kusajiliwa watawashauri kufanya hivyo ili kukidhi matakwa ya sheria. 

MAKUSANYO YA SERIKALI 
Desemba mwaka jana, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikusanya Sh. trilioni 1.3 Novemba na Desemba makusanyo hayo yalipanda na kufikia Sh. trilioni 1.4, huku sehemu ya fedha za miezi hiyo pamoja na mambo mengine zikitumika kuanzisha mpango wa elimu bure. 

Januari kiasi hicho kilishuka mpaka Sh. trilioni 1.06 na malngo ya Februari ni Sh. 1.03. 

MATUMIZI YA FEBRUARI 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, alieleza kuwa kwa Februari, mwaka huu, serikali imeweza kutumia zaidi ya Sh. trilioni moja katika miradi na sekta mbalimbali. 

Baadhi ya sehemu ya fedha hizo, Sh. bilioni 18.7 zimepekwa kutekeleza mpango wa elimu bure, Sh.bilioni 1.65 mafunzo kwa vitendo katika vyuo 35, Sh. milioni 29.1 kununulia vifaa, Sh. milioni 1.49 zilitumika kulipa posho, Sh. milioni 402.1 zilitumika kulipia posho kwa wanafunzi. 

Pia Sh. bilioni 573.2 zilitumika kulipa mishahara kwa watumishi wa umma, Sh. bilioni 842.1 zililipa deni la taifa, Sh. bilioni 81.23 kulipa deni la mifuko ya hifadhi ya jamii, Sh. bilioni 166.1 zilitumika katika miradi ya maendeleo, Sh. bilioni 2.078 zilipelekwa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). 

Sh. bilioni 7.115 katika sekta ya maji na Sh. bilioni 58.168 sekta ya barabara, Sh. bilioni 40.73 sekta ya ujenzi na Sh. bilioni 16.46 zilipelekwa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Sh. bilioni 20.1 sekta ya umeme, Sh. bilioni 2.034 sekta ya reli na Sh. bilioni 12.3 sekta ya mahakama.

CHANZO: NIPASHE

Cement ya Dangote Yaanza Kusambaza Tanzania...Hii ndo Bei ya Mfuko Mmoja wa Cement


Kile kiwanda kikubwa cha Africa mashariki na Africa kwa ujumla kwa mara ya kwanza kimeanza kuzalisha kusambaza cement jana tar 21/02/ 2016.

Kiwanda hicho ambacho ni tegemeo jipya kwa waakazi wa mikoa kusini Mtwara na Lindi kiliahidi ajira nyingi ya wakaanzi wa mikoa hiyo na watanzania kwa ujumla
Cement tayari iko maduka kwa bei nafuu ya sh 13,500 tofauti na cement ya viwanda vingine.

Tunawakaribisha wateja wa cement hiyo na wenye magari makubwa kufungua office mkoani Mtwara ili kuongeza ajira za madereva hapa mkoani

MKE WA KAFULILA ( JESCA KISHOA ) ATAKA DR. MWAKYEMBE NAYE AKAMATWE NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSIKA NA SAKATA LA MABEHEWA MABOVU

Monday, February 15, 2016


Mbunge wa Viti Maalumu, mkoani Singida Jesca Kishoa(CHADEMA), amesema aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe na Katibu Mkuu wake, wanapaswa kufikishwa mahakamani katika sakata la mabehewa mabovu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,  Kishoa alisema viongozi hao, pia aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha wakati huo, naye afikishwe mahakamani kwa sababu ndiye alikuwa mlipaji Mkuu wa Serikali.

Alisema ni aibu Kiti cha Spika kumfukuza mbunge bungeni akidaiwa kuzungumza uongo kabla ya kudai ripoti ya mabehewa ili kujua ukweli wa jambo hilo ni upi.

Aliongeza kuwa, Katibu Mkuu huyo alilipa fedha asilimia 100 kinyume cha sheria wakati Dkt. Mwakyembe ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, aliruhusu mabehewa yanunuliwe.

"Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi naye awajibishwe kwa kosa hilo kama Mtendaji Mkuu wa Wizara...mabehewa hayo yalipokewa kwa mbwembwe lakini kasoro zake zinatokana na zabuni ya utengenezaji wake kutozingatia viwango.

"Kampuni ya Hindustan Engineering haikufanyiwa uchunguzi kuhusu rekodi na uwezo wake, malipo yalifanyika kwa asilimia
100 kabla ya mabehewa hayajawasili nchini," alisema.

Alisema umma unashuhudia baadhi ya vigogo wa TRL wanafikishwa mahakamani kutokana na sakata la mabehewa hayo na kusisitiza sheria ichukue mkondo wake kwa wote waliohusika si  kuwashtaki wachache wakati Mawaziri wanaachwa.

Kishoa ambaye ni Mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alisema hakuna mtu mwenye uhakika kwamba mabehewa mabovu ni 25 kati ya 275.

"Nani ana uhakika kwamba waliokamatwa ndio wanahusika peke yao, haiwezekani Serikali ikajichunguza yenyewe, kujishughulikia yenyewe kwa kuamua nani imtoe kafara, nani imlinde wote, wote washtakiwe kama ilivyo kwa wengine," alisema Kishoa.

Kishoa alihoji kwanini ripoti ya mabehewa inaendelea kufichwa na haifikishwi bungeni ili Bunge liweze kuisimamia Serikali jambo ambalo halitoi picha kwa Bunge la 11.

DK. KIGWANGALLA AUPA SIKU 90 UONGOZI WA HOSPITALI YA MKOA WA NJOMBE-KIBENA KUBORESHA HUDUMA ZAKE LA SIVYO


Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akikagua eneo la kutolea huduma ikiwemo wagonjwa wanaoingia kumuonna Daktari. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Njombe).

Uongozi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe umepewa muda wa siku 90 kurekebisha mapungufu ya utoaji wa huduma za afya, lazima hospitali hiyo itafungwa.
Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na viongozi Mganga Mkuu wa Mkoa, Samwel Mgema na na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Imelda Mwenda na watumishi wa hospitali hiyo.
Dkt. Kigwangalla alitoa agizo kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa hospitali, vituo vya afya na zahati  ili kuweza kubaini changamoto na mafanikio waliyoyapata baada maagizo mbalimbali kutolewa na Serikali.
Miongoni mwa maagizo hayo ni uboreshaji wa huduma kwa kuwepo na vifaa tiba na vya maabara za  kisasa, dawa za kutosha, kuaanza malipo ya mtandao.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alibaini kwamba hospitali hiyo haina  baadhi ya vifaa vya maabara, ambavyo ni muhimu kwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali, ikiwemo mashine ya CT-Scan na kuwepo kwa vifaa vibovu ambayo havijafanyiwa matengenezo, ukiwemo mfumo mbovu wa ukusanyaji taka ngumu na nyepesi.
“Sijaridhishwa na uendeshaji wa hospitali hii na utoaji wa huduma zinazotolewaa ninakuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya, John Luanda kurekebisha mapungufu yaliyopo baada ya miezi mitatu nitarudi nikikuta huduma bado hairidhishi nitakifunga kituo.,” alisema Dkt.Kigwangalla.
Aliongeza kuwa akikuta huduma hadhirishi atafunga hospitali hiyo licha ya kuwa ya Serikali, hivyo hatasubiri kutumbuliwa jipu.
Dkt. Kigwangalla aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuandaa mpango kazi na mkakati wa kuboresha mapungufu yaliyopo katika hospitali hiyo na kuuwasilisha kwake.
Aliutaka uongozi wa hospitali huo kujenga chumba cha upasuaji cha wakina mama na watoto.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Njombe, Mgema alisema watatekeleza maagizo hayo.

SERENGETI BREWERIES LIMITED JOB VACANCY - APPLY HERE.

Friday, February 12, 2016


OLE PROFILE
Job Title: Area Sales Executive (L6)
Reports To: AREA SALES MANAGER

Context/Scope:

Serengeti Breweries Ltd (SBL) operates exclusively in Tanzania and is the 2nd largest beer company with a market share of 17%. SBL is a subsidiary of East Africa Breweries Ltd (EABL) – which is in turn partly owned by one of the world’s biggest alcoholic beverage companies, Diageo. The company is an integrated demand/supply business with 3 operational breweries in Dar and Mwanza, and a third one in Moshi, which is situated in the northern part of the country near the Kenyan border. SBL’s flagship brand is Premium Serengeti lager, which accounts for 85% of SBL sales volumes. The other beer brands are Tusker, Tusker Malt and Pilsner.

SBL’s 2 fully operational breweries in Dar es Salaam and Mwanza have a combined capacity of 1 m Hls. The 3rd brewery with a capacity of 0.5m Hls is in Moshi.
Market Complexity:

SBL operates in a competitive environment and in a vast geography. The main player in the beer industry is Tanzania Breweries Ltd. (TBL), a subsidiary of SABMiller, who until recently were a third party manufacturer of EABL brands Tusker, Pilsner and Guinness. As a result of the cessation of the agreement between TBL and EABL, there is heightened competitive activity in that market.
Inflation rates remain high in Tanzania (7.5% expected in F11) and average income per capita is less than 1 USD per day. The GDP growth is estimated at 6.4% and is expected to grow to 7.1% as investment, trade and tourism pick up. There is growing consumer affluence and consumerism, giving rise to greater opportunities in our product categories.

Purpose of Role:
Manage the assigned Area Distributor’s territory in terms of achieving the primary and secondary sales targets and distribution kpi’s. Lead and motivate Area Distributors, VSM’s and their other staff in his assigned territory to achieve the planned volume, share and revenue targets

Accountabilities
To lead, motivate, coach and effectively manage the Distributors Local Sales force,
Represent SBL in the territory and build great business relations with the top customers
Attainment of his/her regions volume and revenue objectives,
Achieve the availability & visibility objectives and standards in his/her territory,
Ensure proper implementation of BTL activities, Consumer promotions and Trade promotions,
Communicate sales and field related problems to the HQ,
Follow up sales and distribution KPI’s closely and take immediate corrective actions,
Actively participate in hiring and performance evaluation of the AD’s field force including distributors sales reps.
Effectively maintain VSM routes, follow-up performance,
Perform daily reporting and make sure SBL code of conduct, policy and procedures are applied seamlessly.

Qualifications and Experience Required:
EDUCATION:

Must be at least college graduate with mathematical and analytical skills, preferably business administration.

PERSONAL ATTRIBUTES:
Must be excellent in interpersonal communication, self-initiator, must be able to work with low supervision, must have an analytical mind and ambitious to reach high targets, must be able to take business related initiatives to produce positive business results. Must always be wearing clean and presentable branded clothing, must be shaved and showered every day as he is representing SBL in front of the distributors, retail customers and consumers.

SKILL SET:
Must have salesmanship skills, communication skills, presentation skills, negotiation skills, basic calculation and mobile device using skills, must be able to drive vehicles in an excellent manner and be able to lift 18 kg crates with no problem.

Simba 5-1 Mgambo JKT, Tanzania Prisons 2-2 Yanga VPL

Thursday, February 4, 2016



LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), imeendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini huku ikishuhudiwa Wekundu wa Msimbazi, Simba, wakizidi kung’ara huku watani zao (Yanga) wakizidi kupunguzwa kasi jana.

Simba wakiwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, waliendelea kutoa vipigo vya mbwa mwizi, baada ya kuwapigisha kwata Maafande wa Mgambo JKT ya Handeni Tanga kwa mabao 5-1.

Ushindi huo wa vijana wa Jackson Mayanja, umekuja siku tano ikitoka kutoa dozi ya mabao 4-0 kwa African Sports kwenye uwanja huo huo.

Katika mchezo wa jana, Simba ilianza mahesabu dakika ya 5 kwa bao la Hamis Kiiza akiitendea haki pasi ya Ibrahim Ajib.

Dakika ya 14, Mwamuzi Emmanuel Mwandembwa wa Arusha aliamuru penalti baada ya beki mmoja wa Mgambo kuunawa mpira katika eneo la hatari, lakini Kiiza alishindwa kuitendea haki.

Kiungo Mwinyi Kazimoto, aliifungia Simba bao la pili dakika ya 28 kwa shuti la mbali.

Mshambuliaji anayekuja juu kwa kasi, Ajib, dakika 42 aliwanyanyua vitini mashabiki wa Simba baada ya kufunga bao safi kwa kuwachambua mabeki watatu na kipa wao Mudathir Khamis, kisha kuunyunyiza mpira kambani.

Hadi mapumziko Simba walitoka uwanjani kifua mbele kwa mabao 3-0 huku wakikosa nafasi nyingi za kufunga.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Mgambo wakilishambulia lango la Simba huku wakishindwa kufunga baada ya mashambulizi yao mengi kuishia mikononi mwa Kipa Agban Vincent .

Dakika ya 77, mtokea benchi Dan Lyanga aliyeingia akichukua nafasi ya Ajib, aliifungia Simba bao la nne kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda kipa Khamis kabla ya Kiiza kukamilisha mahesabu kwa bao la tano dakika ya 83.

Watoto wa ‘Mchawi Mweusi’ Bakari Shime, Mgambo, walijipatia bao la kufutia machozi dakika ya 88 likifungwa na Full Maganga akimalizia pasi ya Ally Nassoro.

Simba: Vincent Angban, Ramadhani Kessi, Abdi Banda, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Xavi Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamis Kiiza, Ibrahim Ajibu, Haji Ugando.


Mgambo JKT: Mudathir Khamis, Bakari Mtama, Salim Mlima, Salim Kipaga, Ramadhan Malima, Henry Chacha, Sunday Magoja, Mohamed Samata, Full Maganga, Ally Nassoro na Aziz Gilla.


Tanzania Prisons 2-2 Yanga
Tanzania Prisons: Beno Kakolanya, Laurian Mpalile,  Benjamin Asukile, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambert Sabiyanka, Fred Chudu, Mohamed Mkopi, Jeremiah Juma na  Leonce Mutalemwa.

Yanga: Deo Munishi, Abdul Juma, Oscar Joshua, Vincent Bosou, Mbuyu Twite, Juma Makapu, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na  Isafou Boubacar.

HII NDIYO KAULI YA LOWASSA LEO KUHUSU UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR


Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch UKAWA, Mh. Edwrad Lowassa amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwaka huu.
 
Mh. Edward Lowassa amesema hayo ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na wazee kutoka chama cha Chadema ambapo amesema anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya mach 20 huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika. 

Aidha amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na uongozi mzima wa UKAWA wako imara katika kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanaznia ambapo pia amemshukuru waziri mkuu kwa kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa fursa ya kuajipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura mapema 25 ,huku pia akiigusia katiba ya Tanzania. 

Kwa mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enec Ngombare wamempongeza Mh. Lowassa kwa na uvumilivu wake baada ya uchaguzi ambapo pia wamemhakikishia kuwa wako pamoja nae katika safari ya kuelekea mwaka 2020. 

Katika mkutano huo pia uliohudhuliwa na kada wa siku nyingi Kingune Ngombare Mwiru, Mh Lowassa amewataka wazanzibar na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu na kuhakikisha wanadumisha amani ya nchi hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi za kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani Zanzibar.
Via>>ITV

Jaji Mutungi Atoa Usajili kwa Chama kipya cha CM-TANZANIA.


VYAMA vya Siasa nchini vimeaswa kuepukana na migogoro na kutumia vikao vyao katika kuendeleza shughuli zao za kisiasa.

Hayo yamesemwa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis Mutungi wakati akikabidhi Cheti cha Usajili wa muda kwa Chama kipya cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA).

Aidha, Jaji Mutungi amevitaka Vyama vya siasa nchini kufanya siasa na sio uanaharakati kwaki kwa kufanya hivyo malengo yao yatatimia na kuifanya Tanzania kuwa na amani.

‘’Msipende kukimbilia kwenye vyombo vya habari mnapokuwa na migogoro bali malizeni tofauti zenu ndani ya vikao vyenu kulingana na Katiba ya Vyama vyenu’’, alisema Jaji Mutungi.

Aliongeza kuwa, Tanzania inapaswa kuwa na vyama vya siasa vinavyojitambua na vinavyojua wajibu wao katika kuleta maendeleo ya Taifa kwani siasa sio chuki wala uasama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA) Bwana Laban Nkembo amesema kuwa, chama hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuiweka Tanzania kimaadili na uwajibikaji kwa kuwa kinabeba mambo makubwa mawili yakiwemo Amani na Upendo.

Ameongeza kuwa, chama chao sio cha Upinzani na kinaheshimu chama kilichopo madarakani hivyo, kinaahidi kushirikiana na Chama Tawala kuenzi mazuri yanayofanywa na chama hicho.

 ‘’Chama chetu sio cha upinzani, tunataka nchi nyingine duniani ziwe zinakuja kujifunza Tanzania kuhusu amani na maendeleo tulionayo’’, alisema Nkembo.

Aidha, amebainisha kuwa, chama chao cha CM-TANZANIA kitatoa ajira za kudumu kwa Wanachama wake na hata kwa wale wasiokuwa wanachama ambapo kimeshaandaa Idara ya usimamizi mzuri wa huduma kwa jamii kama vile Wazee, Wajane, Walemavu pamoja na Yatima.

CM-TANZANIA ni Chama cha 23 kupokea usajili baada ya Vyama vingine vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu.
 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU