ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

UMOJA WA ULAYA WAPONGEZA HATUA ZA DKT, MAGUFULI.

Tuesday, May 3, 2016

Umoja wa Mataifa ya Ulaya umepongeza hatua zinazochukulia na rais Dkt. John Magufuli,katika kudhibiti vitendo vya rushwa nchini na kuahidi kutoa misaada zaidi ili kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.



Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Mwanza na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguezi,Alvaro Rodriguez, pamoja na Mkuu wa idara ya siasa na mawasiliano wa umoja wa ulaya walipomtembelea Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.
Pamoja na mambo mengine Umoja huo wa Ulaya umetembelea mkoa huo kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji ambapo umeiomba serikali ya Tanzania kuondoa urasimu katika upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.
Licha ya Kupongeza hatua hizo za rais John Magufuli katika kupambana na rushwa Ujumbe huo wa Umoja wa ulaya umetaka serikali iweze kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza katika kuchangamkia fursa za miradi inayofadhiliwa na Umoja huo lakini pia ni njia moja wapo ya kudumisha mahusiano ya Kimataifa.

Ujumbe huo umetembelea baadhi ya miradi wanayoifadhili mkoani humo ikiwemo mradi wa maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mwanza pamoja na mradi wa kuongeza thamani ya ngozi katika chuo cha Teknolojia DIT tawi la Mwanza.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU