Jeshi la Marekani linaangalia uwezekano wa kufungua maeneo 11 ya kituo cha pili barani Afrika kwa mujibu wa msemaji wa AFRICOM. Kanali Mark Cheadle, alizungumza na sauti ya Amerika- VOA mjini Brussels hapo Jumanne lakini
hakuelezea maeneo yapi jeshi linafikiria uwezekano wa kuwa na kituo cha pili, zaidi ya kuelezea kwamba Nigeria sio mojawapo.
Marekani kwa sasa ina kituo kimoja cha kijeshi katika taifa la Djibouti huko Afrika ya mashariki. Vikosi vya Marekani pia vipo nchi kavu nchini Somalia ili kusaidia mapigano ya kieneo dhidi ya kundi la wanamgambo wa al-Shabaab na nchini Cameroon ili kusaidia juhudi za mataifa mbali mbali kupambana dhidi ya kundi la Boko Haram lenye makao yake nchini Nigeria.
No comments:
Post a Comment