Serikali imesema itaanza kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kukipa kila kijiji nchini Sh milioni 50 katika mwaka wa fedha wa 2016-2017.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Sera, Uratibu, Bunge la Walemavu, Antony Mavunde alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo.
Bulembo alitaka kujua ahadi ya Sh milioni 50 kwa kila kijiji itatekelezwa lini.
Mavunde alisema ahadi ya Rais Magufuli ya kila kijiji kupewa Sh milioni 50 itaanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2016-2017.
Alisema utaratibu wa kugawa fedha hizo unaandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
‘’Pamoja na mikakati yote hiyo vigezo ambavyo vimekuwa vikitumika katika kutoa mikopo na mitaji kwa vijana ni umri usiozidi miaka 35 ambavyo ni kujiunga na Saccos za vijana za wilaya na kuunda vikundi na kuvisajili kisheria,” alisema.
Alisema ili kuhakikisha vijana wanakuwa wajasiriamali na wanaweza kupatiwa mikopo na mitaji, serikali imejiwekea mikakati ya kutambua vijana na mahitji yao katika ngazi mbalimbali na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi mbalimbali ya vijana.
No comments:
Post a Comment