ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

27 WAITWA STARS CANAVARO,DIDA NDANI, CHIPUKIZI WAPEWA KIPAUMBELE

Wednesday, May 18, 2016


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii, Dar


Kocha mkuu wa timu ya Taifa'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa imetangaza kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya utakaopigwa Mei 29 jijini Nairobi.


Akitaja majina hayo kocha Mkwasa ameonekana akiwapa kipaumbele vijana huku akimrudisha Nadir Haroub 'Canavaro' na golikipa wa Yanga Deogratius Munish 'Dida'.


"Tumeamua kuangalia wachezaji wachanga na vijana hasa katika kujenga timu ambapo tunaweza kutumia mfumo wowote,"amesema Mkwasa.


Mkwasa amesema wachezaji hao walioitwa waliweza kufanya vizuri kwenye mechi zao katika ligi kuu na wameonyesha uwezo wa hali ya juu kwahiyo imani yake wanaweza kufanya vizuri.


Wachezaji walioitwa ni magolikipa 3 Deogratius Munishi 'dida'(Yanga) Aishi Manula (Azam) Beno Kakolanya (Prison) mabeki ni AggreyMorris (Azam) Mwinyi Haji (Yanga) Mohamed Hussein (Tshabalala),Juma Abdul (Yanga) Erasto Nyoni (Azam) Nadir Haroub 'canavaro' (Yanga) David Mwantika(Azam) na Vicent Andrew 'dante' (Mtibwa)


Kwa upande wa viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba) , Jonas Mkude (Simba) ,Himid Mao (Azam) , Hassan Kabunda (Mwadui), Shiza Kichuya (Mtibwa) Mohamed Ibrahim (Mtibwa) Ismail Juma (JKU) Farid Mussa (Azam) na Juma Mahadhi (Coastal Union)


Washambuliaji ni Mbwana Samatta (Genk ubelgiji), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), Jeremia Juma (Prisons) Deus Kaseke (Yanga) Ibrahim Ajib (Simba) John Bocco (Azam) na Elius Maguli ( Stand United).


Mkwasa amesema kuwa wachezaji hao wanatakiwa kuingia kambini siju ya Jumatatu Mei 23 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuumana na Misri kufuzu mataifa Afrika AFCON Juni 04.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU