ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

BREAKING NEWS:KIVUMBI KIMEWAKA MAWAZIRI 7 WA RAIS MAGUFULI WAKUTANA NA RUNGU ZITO LA John Pombe Magufuli

Sunday, September 18, 2016

Mawaziri hao huenda miongoni mwao wakajikuta katika hatari ya kukabiliana na rungu zito la Rais John Magufuli, ambaye alishasisitiza mara kadhaa kuwa daima huwa hana subira na watu wanaokwenda kinyume cha taratibu za uongozi, ikiwamo kuwatumbua bila kujali majina yao. 
Tishio hilo la hatima ya baadhi ya mawaziri katika serikali ya sasa ya awamu ya tano, linatokana na kile alichokieleza jana Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuwa
baadhi ya wasaidizi hao wa Rais wamekuwa wakikacha majukumu yao bungeni kwa kutoonekana pasi na sababu za msingi. 
Aidha, katika kundi hilo, wamo pia wabunge waliochaguliwa na wananchi katika majimbo mbalimbali nchini ili wawawakilishe bungeni lakini badala yake, miongoni mwao wapo waliokubuhu kwa kukacha wajibu wao huo wa msingi. 
Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana, Spika Ndugai aliwashukia mawaziri wasioshiriki vikao vya kamati za kadumu za chombo hicho cha kutunga sheria na kuweka wazi kuwa sasa anakusudia kuwashtaki kwa kuwasilisha majina ya wale waliokubuhu kwa vitendo hivyo kwa Rais Magufuli ili wachukuliwe hatua. 
Aidha, Ndugai aliwaonya wabunge watoro na kutahadharisha kuwa atawashtaki kwa wananchi na vyama vyao vya siasa iwapo wataendelea na tabia hiyo.
Ndugai aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana wakati wa kuhitimisha mkutano wa nne wa Bunge la 11 ulioanza Septemba 6, mwaka huu.
Spika huyo ambaye aliingia kumalizia kikao hicho cha mwisho dakika chache kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kupewa fursa ya kutoa hoja ya kuahirisha Bunge, alionekana akizungumza kwa umakini mkubwa.
Alisema utoro miongoni mwa mawaziri na wabunge umekuwa ukiathiri utendaji kazi wa kamati hizo za kudumu za Bunge.
"Mahudhurio kwenye kazi za kamati, ukiondoa kamati ya PAC (Hesabu za Serikali), kamati nyingi zilizobaki mahudhurio yake si mazuri sana. Si mazuri kwa mawaziri, si mazuri kwa wabunge baadhi. Ninaomba kule tunakokwenda tuzingatie sana mahudhurio kwa pande zote mbili," alisema.
Katika kuonyesha kuwa Bunge linataka mawaziri na wawakilishi hao wa wananchi kuchapa kazi, Ndugai alisema atayapeleka majina ya mawaziri watoro kwa ‘Namba Moja’, akimaanisha Rais Magufuli.
Aliwataka mawaziri kuhakikisha wanawajibiki ipasavyo na kupanga ratiba zao mapema ili kuepuka kuathiri vikao vya kamati za kudumu za Bunge.
"Tumetengeneza orodha ya watoro. Mawaziri watoro, wabunge watoro kwenye kamati, lakini nimesema niitunze tuangalie na kwenye kikao kijacho. Kama watoro hao wataendelea, basi tutawaambia waajiri wao kwa maana ya wapigakura wenu, kwa maana ya vyama vyenu, kwamba mbunge huyu na mbunge huyu kazi zetu kwenye kamati za Bunge hafanyi, ili hivyo vyama vijue.
Na kwa upande wa mawaziri, basi tutamwambia 'Namba Moja' kwamba hawa hawawajibiki. Kwa hiyo, natoa nafasi kwa mawaziri na wabunge kuhakikisha mnapanga ratiba zenu mapema," alisema 
Aliwataka mawaziri na wabunge kuhakikisha wanazingatia ratiba aliyoitoa jana ya vikao vya kamati za Bunge vitakavyofanyika ndani ya siku 15 kuanzia Oktoba 17, yaani siku 14 kabla ya kuanza kwa mkutano wa tano wa Bunge la 11 ambao pamoja na mambo mengine, utajadili taarifa za uchambuzi wa ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Uchambuzi wa ripoti za CAG unafanywa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mitaa (LAAC) na ile ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo pia katika mkutano ujao wa Bunge utakaoanza Novemba Mosi, inatarajiwa kuanika ripoti ya uchunguzi wa mkataba tata wenye thamani ya Sh. bilioni 37 kati ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd.
AMPONGEZA MBOWE
Katika hatua nyingine, Ndugai ambaye alipishwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, kuongoza kikao cha jana, alimpongeza Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kutokana na ushiriki wa wabunge wa upinzani katika mkutano wa nne, tofuati na mkutano wa tatu ambao waliususa.
"Nimpongeze sana Waziri Mkuu ambaye anaongoza wabunge wengi hapa, lakini nimpongeze pia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa kuyaongoza makundi yao vizuri.
"Tumefanya kazi vizuri bila migogoro yoyote katika mkutano huu wa nne. Watanzania wanapenda hali hii. Watanzania hawapendi kuona vurugu kubwa, msambaratiko, maana msambaratiko ukianzia hapa unakwenda hadi kwa wananchi wetu. Umoja ukiwa hapa, unaenda na kwa wananchi wetu.
"Kwa hiyo, nawapongeza sana kwa jinsi mlivyoongoza mambo yenu katika kipindi hiki kwa salama na amani. Tuendelee na utaratibu huu,” alisema huku wabunge wakipiga kofi.
UFAFANUZI NJE YA BUNGE
Alipotafutwa na Nipashe kwa simu baada ya kuahirishwa kwa Bunge, Ndugai hakuwa tayari kuanika majina wala idadi ya mawaziri ambao hawahudhurii vikao vya kamati za Bunge.
Hata hivyo, alisema mawaziri wengi wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa kamati hizo na wameelekeza nguvu nyingi kwenye shughuli za kiserikali. Spika huyo alibainisha kuwa baadhi yao hawakuhudhuria hata kikao kimoja cha Bunge.
"Wanabadili tarehe mara leo wana udhuru huu, kesho wana udhuru huu, inakuwa inasumbua. Kwa sababu ya 'commitment' walizo nazo serikalini ambazo wamezipa kipaumbele zaidi kuliko shughuli za Bunge," alisema Ndugai.
"Unakuta labda ana mkutano wa kufungua Arusha au Mwanza, lakini siku hiyo anatakiwa bungeni kwa ajili ya jambo fulani kwenye kamati ambayo ni ratiba ambayo anakuwa ameshaipata tangu zamani,” alisema. 
Kuhusu mahudhurio ya wabunge kwenye kamati na vikao vya Bunge, Spika alisema ni asilimia 60 tu ya wabunge hushiriki vikao vinavyofanyika asubuhi, wakati asilimia 40 hushiriki vile vya jioni. 
"Kila kamati ina mahudhuri ya tofauti tofauti na zingine, lakini kwa ujumla, wastani ni kama asilimia 40 hawahudhurii kwa kamati zote, isipokuwa Kamati ya Fedha na PAC, wao ni asilimia 90 ya mahudhurio," alisema.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU