Katika hatua ya kushangaza, kiongozi wa visiwa vya Sao Tome na Principe, mojawapo ya mataifa madogo zaidi barani Afrika, amesusia awamu ya pili ya uchaguzi nchini humo.
Rais Manuel Pinto da Costa amesema uchaguzi huo hauwezi kuwa
wa haki na akawahimiza wafuasi wake kutoshiriki.
Aliwataka wafuasi wake kutoshiriki uchaguzi huo wa Jumapili baada ya kupata chini ya robo ya kura zilizopigwa katika duru ya kwanza.
Rais huyo alipata 24.8% ya kura zilizopigwa katika awamu hiyo ya kwanza tarehe 17 Julai naye mpinzani wake Evaristo Carvalho akapata 49.8%. Alisema uchaguzi huo wa kwanza ulikumbwa na udanganyifu.
Taarifa zinasema wengi wa wafuasi wake walisusia uchaguzi huo wa kwanza.
Bw Carvalho, ambaye alikuwa spika wa bunge na pia waziri mkuu, anaonekana kuhakikishiwa ushindi.
Bw Pinto da Costa ameongoza kwa miaka mitano.
Awali, aliongoza taifa hilo wakati wa utawala wa chama kimoja kuanzia 1975 hadi 1991 alipofanikisha kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
Taifa hilo, ambalo lilitawaliwa na Ureno, linajumuisha visiwa viwili vikubwa Sao Tome na Principe pamoja na visiwa vingine vidogo.
No comments:
Post a Comment