ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

YANGA ‘WAMPA’ MANJI TIMU KWA MIAKA 10 Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ

Saturday, August 6, 2016

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM WANACHAMA wa Yanga wamekubali kumkodisha klabu hiyo Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kwa miaka 10 kuanzia leo. Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu wa dharula uliofanyika leo ukumbi wa
Diamond jubilee, Dar es Salaam. Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama. Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini ya Manji. Aidha, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu, Francis Kifukwe alisema baada ya wanachama kuridhia mpango huo, wao wanampa pia ridhaa hiyo Manji. 


Mkutano wa Yanga unaendelea hivi sasa Diamond Jubilee na awali wanachama watatu wa klabu hiyo, Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashim Abdallah walifukuzwa. Manji aliwaambia wanachama hayuko tayari kufanya kazi na Wajumbe hao wa Kamati ya Utendaji na akaomba wanachama wanaowataka wajitokeze kupiga kura, lakini hakuna aliyeinuka. Baada ya kurudia kuita mara tatu, Hashim pekee kati ya watatu hao ambaye alikuwepo mkutanoni ukumbi wa Diamond Jubilee, akainuka na kuondoka. Mwanachama mwingine, Siza Lyimo ambaye Manji alitaka aondoke, yeye aliomba msamaha na wanachama wakamsamehe na Mwenyekiti huyo akabariki msamaha huo. Mkemi na Nyenzi hawakutokea kwenye Mkutano huo.

Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU