Habari za Mahusiano Kila siku
JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE
ETC RADIO ONLINE LIVE
http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/
TCRA yaiadhibu EATV kutokana na kucheza video ya wimbo ‘Panya’ wa Bracket, nayo E-FM yapata adhabu
Saturday, May 28, 2016
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekiadhibu kituo cha runinga cha East Africa Television (EATV) kulipa faini ya Tsh 3 milioni kutokana na kukiuka kanuni za utangazaji baada ya kuicheza video y
China yakana kuuza nyama ya binaadamu Afrika
Monday, May 23, 2016
Wizara ya maswala ya kigeni nchini China imekana ripoti kwamba kampuni za chakula nchini humo zinaweka nyama ya binaadamu na kuuza barani Afrika kama nyama ya ng'ombe.
Chombo cha habari nchini humo Xhinua kimesema kuwa jarida moja nchini Zambia lilimnukuu kimakosa mwanamke mmoja ambaye hakutajwa anayeishi China.
Alisema kuwa kampuni za China zilikuwa
Manchester United yamfuta kazi Louis van Gaal
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United, huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake.
Raia huyo wa Uholanzi anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya mitatu.
Kitengo cha habari za michezo cha
Rais Magufuli Akutana Na Waziri Mkuu, Jaji Mkuu Na Kamishna Mkuu Wa TRA Ikulu Jijini Dar Es Salaam Mei 23,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika
Marekani yaangalia uwezekano kufungua vituo zaidi vya kijeshi Afrika
Wednesday, May 18, 2016
Jeshi la Marekani linaangalia uwezekano wa kufungua maeneo 11 ya kituo cha pili barani Afrika kwa mujibu wa msemaji wa AFRICOM. Kanali Mark Cheadle, alizungumza na sauti ya Amerika- VOA mjini Brussels hapo Jumanne lakini
Upinzani Wamtega Rais Magufuli....Watumia Njia Mbadala Bungeni Kukumbushia Uuzwaji wa Nyumba za Serikali, Wadai MV Dar es Salaam Ni Jipu Lililoiva
Kambi ya Upinzani imelizidi maarifa Bunge na kurejesha sakata la kuuzwa nyumba za Serikali ambalo juzi lilisababisha kiti cha Spika kuagiza yaondolewe maneno yanayomtaja Rais katika hotuba ya maoni mbadala.
Juzi, Kamati ya Kanuni za Bunge ilihariri hotuba ya msemaji wa
KIKOSI KAMILI CHA YANGA DHIDI YA GD SAGRADA ESPERANCA.
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van De Pluijm ametoa kikosi kitakachovaana na timu ya GD Esperanca mechi ya kombe la Shirikisho Afrika itakavaana majira ya 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kikosi cha Yanga ni
1. Deogratius Munishi
2. Juma Abdul
3. Oscar Joshua
4. Vicente
27 WAITWA STARS CANAVARO,DIDA NDANI, CHIPUKIZI WAPEWA KIPAUMBELE
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii, Dar
Kocha mkuu wa timu ya Taifa'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa imetangaza kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya utakaopigwa Mei 29 jijini
WABUNGE WATWANGANA NGUMI BUNGENI.
Tuesday, May 3, 2016
Wanachama wa chama tawala cha Uturuki cha AK na chama kinachoungwa mkono na Wakurdi wamepigana ngumi bunge kuhusiana na
WAZIRI NAPE NNAUYE AENDELEZA MCHAKAMCHAKA NA WAHANDISHI WA HABARI.
Na Daudi Manongi-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amesema kuwa atahakikisha heshima ya tasnia ya habari inarudi baada ya kupitishwa kwa mswada wa sheria ya huduma za vyombo vya Habari.
Waziri Nape ameyasema hayo alipokuwa katika katika ziara mkoani Mara na Shinyanga na kutembelea maeneo yanayohusu sekta za
HUU NDIO MWAKA AMBAO SERIKALI ITATOA MILIONI 50 KWA KILA KIJIJI.
Serikali imesema itaanza kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kukipa kila kijiji nchini Sh milioni 50 katika mwaka wa fedha wa 2016-2017.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Sera, Uratibu, Bunge la Walemavu, Antony Mavunde alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo.
Bulembo alitaka kujua ahadi ya Sh milioni 50 kwa kila kijiji itatekelezwa lini.
Mavunde alisema ahadi ya Rais Magufuli ya kila kijiji kupewa Sh milioni 50 itaanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2016-2017.
Alisema utaratibu wa kugawa fedha hizo unaandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
‘’Pamoja na mikakati yote hiyo vigezo ambavyo vimekuwa vikitumika katika kutoa mikopo na mitaji kwa vijana ni umri usiozidi miaka 35 ambavyo ni kujiunga na Saccos za vijana za wilaya na kuunda vikundi na kuvisajili kisheria,” alisema.
Alisema ili kuhakikisha vijana wanakuwa wajasiriamali na wanaweza kupatiwa mikopo na mitaji, serikali imejiwekea mikakati ya kutambua vijana na mahitji yao katika ngazi mbalimbali na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi mbalimbali ya vijana.
UMOJA WA ULAYA WAPONGEZA HATUA ZA DKT, MAGUFULI.
Umoja wa Mataifa ya Ulaya umepongeza hatua zinazochukulia na rais Dkt. John Magufuli,katika kudhibiti vitendo vya rushwa nchini na kuahidi kutoa misaada zaidi ili kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez
Pongezi hizo
Swansea yaichapa Liverpool 3-1
Monday, May 2, 2016
Andre Ayew akifunga bao la pili dhidi ya Liverpool
Mshambulizi wa Black Stars ya Ghana Andre Ayew alifunga mabao mawili na kuisadia timu yake ya Swansea kujihakikishia nafasi katika ligi kuu ya Uingereza msimu ujao.
Ayew alifunga mabao hayo Swansea City ilipojifurukuta na kuiadhibu Liverpool 3-1.
Ayew alifungua kibano hicho kwa mkwaju wa kichwa kabla ya Jack Cork kufuma kimiani mkwaju ulioipa swansea uongozi wa mabao mawili kwa nunge kufikia muda wa mapumziko.
Hata hivyo vijana wa Jurgen Klopp walirejea uwanjani kwa kishindo.
Christian Benteke alirejeshea Liverpool matumaini kwa kufunga bao mapema katika kipindi cha pili.
Lakini Ayew akawazimia nuru kabisa katik mechi hii alipofunga bao lake la tatu na la ushindi dakika mbili tu baadaye kunako dakika ya 67.
Masaibu ya Liverpool yaliongezeka Brad Smith alipooneshwa kadi yake ya pili ya njano na hivyo kulazimika kuiaga mechi hiyo.
Kufuatia kichapo hicho Liverpool sasa haina budi kujinga ukanda iliangalau waweze kushinda kombe la Europa iwapo bado wanamatumaini ya kushiriki katika kombe la mabingwa barani ulaya mwakani.
Kwa upande wao Swansea, ambao wanaorodhewshwa katika nafasi ya 13 wamejizolea alama 11 zaidi ya Sunderland ambayo iko katika hatari kubwa ya kushushwa daraja msimu ujao.
Magufuli apunguza kodi ya mapato na 2%
Huku wafanyikazi kote duniani wakiadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, nchini Tanzania, wafanyikazi wanakila sababu ya kutabasamu.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaongezea wafanyikazi wote nchini humo asilimia mia mbili 2% mishahara.
Katika hotuba ya kuadhimisha siku ya wafanyikazi, bw Magufuli alitangaza kupunguzwa kwa kodi ya mapato PAYE kutoka asilimia 11% hadi asilimia 9%.
Hii inamaanisha kuwa kila mfanyikazi atapata ongezeko la mapato yake kwa asilimia 2%.
Magufuli alitangaza kauli hiyo kufuatia ombi la wafanyikazi kupitia kwa katibu mkuu bwana Nicholus Mgaya la kutaka wanusuriwe makali ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu.
Aidha rais Magufuli alisema anatimiza ahadi aliotoa kwa wapiga kura wakati wa kampeini kuwa endapo watamchagua angefanya kila jitihada kuwapunguzia mzigo wa kodi wafanyikazi wa Tanzania.
Kuhusu ongezeko la mshahara wa chini zaidi atakaolipwa mtanzania bw Magufuli amewasihi wampe muda kidogo akomeshe rushwa na kuimarisha uchumi wa taifa
''Pamoja na uamuzi huo, Rais Magufuli pia amewaahidi wafanyakazi kuwa baada ya kupunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi, serikali yake itafanyia kazi mapendekezo ya kuongeza mishahara''
''aidha, amewataka wafanyakazi kuunga mkono juhudi za kuwafichua wanaozalisha wafanyakazi hewa, huku akibainisha kuwa mpaka kufikia jana tarehe 30 Aprili, 2016 jumla ya wafanyakazi hewa waliobainika walikuwa 10,293 ambao kwa mwezi mmoja tu wamelipwa shilingi bilioni 11.6.''
Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, ikulu Dodoma Gerson Msigwa ilisema.
Magufuli alitangaza kauli hiyo kufuatia ombi la wafanyikazi kupitia kwa katibu mkuu bwana Nicholus Mgaya
BREAKING NEWS: NJAMA ZA KUKWAMISHA SERIKALI YA MAGUFULI ZANASWA,MAZITO YAFICHUKA
WAFANYAKAZI WAANGUA VILIO KUTOKANA NA MANYANYASO KAZINI WAKATI WA MAADHIMISHO YA MEI MOSI MBELE YA MKUU WA MKOA TANZANIA
Sunday, May 1, 2016
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
Dar/Zanzibar/Mikoani. Wakati Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akijitetea kwa kutoongeza mshahara, Bara wafanyakazi wamelia kunyanyaswa na wawekezaji, huku walimu watoro wakinyooshewa kidole.
Akizungumza katika maadhimisho hayo ya Mei Mosi, Dk Shein (pichani) aliwaacha hoi wafanyakazi pale aliposema kuwa katika utekelezaji wa ahadi ya kuimarisha masilahi yao, hawezi kufanya usanii na hawezi kuahi
Dar/Zanzibar/Mikoani. Wakati Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akijitetea kwa kutoongeza mshahara, Bara wafanyakazi wamelia kunyanyaswa na wawekezaji, huku walimu watoro wakinyooshewa kidole.
Akizungumza katika maadhimisho hayo ya Mei Mosi, Dk Shein (pichani) aliwaacha hoi wafanyakazi pale aliposema kuwa katika utekelezaji wa ahadi ya kuimarisha masilahi yao, hawezi kufanya usanii na hawezi kuahi
Subscribe to:
Posts (Atom)