ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

WAKENYA WANAVYOMZUNGUMZIA RAIS MAGUFULI

Wednesday, November 25, 2015


Na Francis Godwin
Unajua nini mtu wangu una kila sababu ya kujivunia kuwa Tanzania wakati na muda kama huu kwani kasi ya Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli inaweka headlines kubwa sana kwa nchi za jirani na si kwa Watanzania pekee!
Nimetembelea mtandao wa kijamii wa Twitter na nimekutana na tweets za Wakenya juu ya Rais Dk. John Pombe Magufuli na kwenye kuzisoma tweets zao nimegundua sifa za Rais Magufuli na maamuzi yake ya kazi toka ameshika rungu la Tanzania zimewafikia.
Wengi wamemsifia na wengine wameandika wakiomba Mungu awape Rais kama Magufuli….. tweets nyingine unaweza kuzisoma kwenye hii post.



Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Rais Dk. John Magufuli amefanya mambo kadhaa ambayo yamewaridhisha na kuwapa moyo Watanzania, mambo hayo ni kama…
1. Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili  ilivumbua vitu vingi na kumpelekea Rais Magufuli kufuta bodi ya Wakurugenzi wa hospitali hiyo pamoja na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk. Hussein Kidanto.
2. Kufuta safari za viongozi kwenda nchi za nje ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa za Serikali.
3. Alielekeza shilingi milion 225 zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla ya Pongezi za Wabunge Dodoma kutumika kununua vitanda vya hospitali na shilingi milion 15 tu ndio zitumike kwaajili ya sherehe hiyo.
4. Jumatatu ya tarehe 23 November 2015, Rais Dk. John Magufuli alitangaza kufuta kwa sikukuu ya Uhuru December 9 na kuagiza fedha za maandalizi ya sikukuu hiyo zitumike kutatua matatizo mengine pia ameagiza siku hiyo itumike kusafisha mazingira ili kupunguza matatizo ya kipindupindu nchini.
Mambo haya machache na makubwa yamewapa faraja kubwa sana Watanzania na kumfanya Rais Magufuli awe topic kubwa kwenye mtandao wa Twitter kwa raia wa Kenya!
Kama kawaida kazi yangu ni kuzinasa zile zote zinazoweka headlines wakati huu na hizi ni baadhi ya#tweets nilizofanikiwa kuzinasa, karibu uzipitie moja baada ya nyingine uone jinsi gani Wakenyawalivyoguswa…

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU