ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

MO APATA TUZO NYINGINE, ADHIHIRISHA TAMAA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA

Saturday, November 28, 2015

Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akitembea kwenye 'Red Carpet' mara baada ya kuwasili katika hotel ya Hilton Sandton jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwenye hafla ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida maarufu la Forbes na kutunukiwa tuzo ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015".(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Modewjiblog team
MFANYABIASHARA na mtu mwenye taasisi ya kusaidia jamii, Mohammed Dewji maarufu kama Mo ametunukiwa tuzo ya jarida maarufu la Forbes ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015" katika hafla iliyofanyika Novemba 27 mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mfanyabiashara huyo pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises T Ltd (MeTL Group) kampuni iliyoanzishwa na na baba yake katika miaka ya 1970 ambayo sasa imekua na kujikita katika viwanda vya nguo, usagaji nafaka, utengenezaji wa vinywaji baridi, usindikaji wa mafuta ya kula, usindikaji wa chai na kuendesha mashamba ya mkonge ambapo tayari anashea ya asilimia 40 ya soko.
Mo ametwaa tuzo hiyo kwa kuwashinda watu watano mashuhuri barani Afrika. Watu hao ni Nkosazana Dlamini Zuma, mke wa Kwanza wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. Mama huyo kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mwingine ni Rais wa sasa wa Nigeria, Muhammadu Buhari aliyetambuliwa kutokana na kuanzisha vita dhidi ya rushwa nchini mwake.
Aidha wapo Arumna Otei, mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia. Pia alikuwemo Mwandishi maarufu wa vitabu wa Nigeria, Chimanda Ngozi Adichie ambaye moja ya vitabu vyake vinaelezea picha halisi ya Afrika inavyofikiriwa duniani.
Akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo hiyo Mo, alisema anatoa tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba uchumi wa nchi.
Mo ambaye kampuni yake ya MeTL inaongoza kwa kutoa ajira nchini, ikiwa imetoa ajira 26,000 kote katika viwanda vyake 31 vilivyopo nchini na katika mataifa matano ya Afrika, alisema amefurahishwa na tuzo hiyo ambayo anaitoa kwa vijana kwa kutambua pia wajibu mkubwa walionao katika kukabiliana na umaskini.
Alisema ajira 26,000 zimegusa watu wengi nchini na kwamba ana matumaini makubwa ya siku za usoni kutoa ajira zaidi kutokana na biashara zake kuendelea kukua.
"Heshima yangu kubwa haitokani na utajiri, maana kama utajiri wako hauna msaada wala kugusa watu masikini hauna maana yeyote, hivyo basi heshima hii ni kutokana na kwanza bidhaa zangu kugusa maisha ya watu kila siku kuanzia sukari na majani ya chai asubuhi pamoja na unga wa ngano, lakini pia chakula cha mchana kwa unga wa sembe, mafuta ya kupikia na maji ya kunywa, bidhaa zote hizo za Mohammed Enterprises zinagusa maisha kila nyakati katika siku.
"Nina viwanda 31 ambavyo vimekuwa vikitengeneza bidhaa za Kitanzania na kuziuza kwa Watanzania kwa bei yenye unafuu mkubwa, mathalani tunauza maji kwa bei chini ya dola moja kwa shilingi za Kitanzania 200, hakuna hata Ulaya, nina kiwanda cha khanga na vitenge ambacho malighafi zake zote ni za Kitanzania, hivyo kuna kusaidia serikali kwa kulipa kodi ipasavyo, lakini pia kusaidia moja kwa moja ajira za Watanzania walio wengi ambao tatizo lao kubwa katika kundi la vijana ni ajira"
Alitumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza baba yake kwa kumwita mjasiriamali shujaa ambaye alitoka kuanzia dereva wa malori baada ya kuhitimu kidato cha nne mwishoni mwa miaka ya 1960 hadi kufikia ubilionea. Alisema alipata maono ya utajiri hasa kutoka kwa baba yake huyo aliyekuwa akimshirikisha biashara tangu akiwa mdogo.
“Mwanaume mwenye ndoto huhitaji mwanamke mwenye maono. Na nimebarikiwa mwanamke ambaye kwa miaka 15 amekuwa akinipa sapoti isiyoyumba.
“Saira, nina shukurani nyingi kwako kwa kuwa nguzo ya familia yetu, mama wa heshima kwa watoto wetu watatu,” alisema Mo kwenye hafla hiyo.
Kwa utulivu, Mo alisema: “Baba, zawadi kubwa ambayo ulinipa katika maisha yangu ni muda wako, na kwa hilo nitakuwa mwenye deni la shukurani kwako siku zote za maisha yangu.”
Mo ambaye moyo wake wa binadamu ulimfanya awanie uwakilishi Jimbo la Singida Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushinda nafasi hiyo na hivyo kuwawakilisha wanasingida kuanzia 2005 na 2015 amesema maisha ni changamoto kubwa inayobadilishwa kwa utumishi wenye nia ya dhati kwa umma.
Alisema alipowania uwakilishi alikuwa na sababu: “Nilikuwa na umri wa miaka 24, nilikwenda Singida kutoa heshima kwenye kaburi la marehemu babu yangu. Sikuwa nimefika huko tangu nilipoondoka nikiwa na umri wa miaka mitatu.
“Nilipokuwa njiani, nilimuona mzee akiwa na maji yenye rangi ya njano, machafu ambayo aliyatumia kwa kunywa. Nilishangaa, maana hali ile sikuwahi kufikiri kama ipo vile. Kipindi hicho nilikuwa nimemaliza Chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani.”
Mo anasema kuwa aliingiwa na hisia kutaka kujua nini hasa alichokuwa anahitajika kufanya, alimfuata yule mzee aliyekuwa na maji yale, alipozungumza naye, aliwazungukia watu wengine na kuridhika kuwa ile ndiyo hali halisi, hapo ndipo fikra ya kwa nini agombee ubunge ilipoanzia.
Anasema kuwa baada ya kujiridhisha hivyo, alirudi kwa mzee wa kwanza, alizungumza naye na kumuuliza ni kwa nini shida ile ilikuwa haizungumzwi kwa upana katika mamlaka husika.
“Nilipojitambulisha yule mzee alisema anamkumbuka babu yangu, kisha akanishauri nigombee ubunge, alinisisitiza mno ili nisaidie kuondoa lile tatizo la watu wa Singida kunywa maji machafu,” alisema Mo.
Anaeleza kuwa alipokuwa njiani kurejea Dar es Salaam, alilifikiria tatizo hilo kwa mapana zaidi, akalifanyia utafiti na kubaini kwamba katika kila watu 10, watatu walikuwa wakipoteza maisha kutokana na maradhi yanayosababishwa na maji machafu.
Anaendelea kusema kuwa aligundua kuwa Singida kulikuwa na tatizo kali la maji safi na salama. Anasema kuwa alibaini uwepo wa tatizo la elimu kuhusu matatizo ya maji.
Jambo lingine ambalo anasema aliligundua ni uwepo wa tatizo la huduma za afya. “Niliwafikiria watoto wangu, jinsi ninavyowapenda, na namna ambavyo kila mzazi anavyompenda mwanaye. Nilipingana na hali kuwa watoto wa Uingereza na Marekani wamependelewa zaidi. Maisha ni sawa bila kujali chochote,” anasema Mo.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU