Na Furaha Eliab, Njombe
CHAMA cha demokrasia na maendeleo Chadema, Jimbo la Njombe kusini kimesema kuwa kimefungua kesi ya kupinga matokeo katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa, na kuwashitaki Mgombea wa CCM, Mwalongo, Mwanasheria wa serikali, na msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe baada ya kufungua kesi hiyo aliye kuwa Mgombea ubunge jimbo la Njombe Kusini Emmanuel Masonga alisema kuwa wameamua kufungua kesi hiyo baada ya kujiridhisha ushahidi walionao utawawezisha kushinda kesi yenye namba 6/2015.
Alisema kuwa wamebaini kuwa katika uchaguzi huo kulikuwa na ukiukaji wa mkubwa wa sheria za uchaguzi tangu kuanza kwa kampeni, uchaguzi hati kutangazwa kwa matokeo.
Alisema kuwa katika kesi hisyo wameamua kumshitaki Mkurugenzi wa uchaguzi, mgombea wa CCM ambaye ni mbunge Edward Mwalongo kutokana na uchaguzi huo ulivyo endeshwa wakati wa kampeni na kipindi cha uchaguzi.
Masonga alisema kuwa wameanda wanasheria wa kutosha ambao watasimamia kesi hiyo na kuwa watatajiwa siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo baada ya kufanyiwa tathimini ya gharama ya uendeshaji na kuhakikishiwa ulinzi wa gharama za kezi.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa ushahidi na vielelezo vyote tayari wanavyo kwaajili ya kuvitoa mahakamani na kuwa hawata weza kuviweka wazi kwa kuwa tayari ni mari ya mahakama kwa sasa tangu wafungue kesi na kuwa vikionyeshwa vinaweza kuwapa ushindi wapinzani wao.
"Mahakama baada ya kujiridhisha na vigezo vya kufungua kesi, walifungua kesi na kuipa namba sita, hivyo watanzania wakae tayari kwa kuwa tutaenda mahakamani na sikotayari kuchukua hongo, katika kesi yetu tumewashitaki watu watatu, wakwanza ni Mwalongo, wapili msimamisi wa uchaguzi na watatu ni Mwanasheria mkuu wa serikali," alisema Masonga.
Alisema kuwa mahakama inaenda kumtangaza mshindi baada ya kushinda kesi hivyo wakazi wa mkoa wa Njombe wakae tayari kuyapokea matokeo.
Aliongeza kuwa kesi yao itaongozwa na mawakili saba, wakiongozwa na Edwin Swale na kuomba wakazi wa Njombe wenye taaluma ya sheria kumuunga mkono.
Aidha mwenyekiti wa kamati ya kusimamia kesi hiyo Emmanuel Filangali alisema kuwa wameamua kuita waandishi wa habari kuwajulisha pale walipo fikia baada ya kwa mara ya mwisho kufikia maamuzi ya kufungua kesi mahakamani.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment