ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

MAKUNDI YA JAMII ASILIA YA WAHADZABE, WABARABAIG, WAMASAI WAIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWATAMBUA KAMA JAMII NYINGINE

Friday, November 27, 2015

Na Andrew Chale, Modewjiblog

Jamii ya watu wa asili na makundi yao wameiomba Serikali ya Tanzania kutambua uwepo wao hapa nchini ikiwemo kuwatangaza kwa mema na kuwasaidia kwa misingi ya haki, hutu na kimaendeleo kama watu wengine wanaotambulika ndani na nje ya mipaka yao.

Hayo yameelezwa mapema leo jijini hapa wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania wakiwemo makabila ya Wa-Akiye,Wa- Hadzabe,Wa- IIparakuyio Masai na wengine wengi.

Akielezea katika uzinduzi huo mmoja wa wajumbe walioandaa taarifa ya Tume hiyo, ambaye anatoka nchini Kenya, katika taasisi ya African Commission on Human and Peoples Rights (ACHPR), Dk. Naomi Kipuri amebainisha kuwa jamii ya watu asilia wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha kutaka kupata haki zao zao msingi na kutambulika zaidi.

“Utafiti tuliofanya jamii ya watu asilia wamekuwa katika malalamiko ya muda mrefu ikiwemo kutaka haki zao za msingi. Ikiwemo masuala ya elimu, makazi na haki zingine. Pia wameomba Serikali kuwatangaza watu hawa wa asilia ili wasionekane wageni kwani jamii nyingi bado hazijawatambua na hata kupelekea kuwavunjia hutu wao” alieleza Dk. Naomi.


Aidha, Dk. Naomi katika uwakilishi wake wa mada kwenye mkutano huo amelezea namna ya jamii inavyoendelea kuwaona watu hao ni tofauti kiasi cha kupelekea watu hao kudumaa na maisha yale yale ya asilia.
“Jamii zingine zinawatenga watu wa jamii ya Wamasai, tumeshuhudia lugha na matamshi kwenye mizunguko ya watu ikiwemo kwenye madaladala, mitaani huku wakimuona Mmasai kama mtu tofauti, sasa katika ripoti hii imeweza kuelezea mambo mengi sana. Ikiwemo suala la Haki ya kuishi, kufanya kazi na mambo yote kama watu wengine” alimalizia Dk. Naomi. 

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri ameeleza kuwa kupitia ofisi yake itahakikisha inashughulikia suala hilo la kuwa karibu na watu asilia na kutambua misingi ya haki zao ambapo amebainisha watu hao wa asilia kwa Tanzania wanafikia makundi zaidi ya sita. 

Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi wa watu hao wa watu asilia wakielezea katika mkutano huo, waliomba na wao na wapate wawakilishi maalum ikiwemo Bungeni ama sehemu za maamuzi ikiwemo Halmashauri na maeneo mengine ya Serikali ilikutambua michakato ya Kimaendeleo kwa kina. “Jambo la ardhi, ndilo linalotuumiza kwa sasa.

 Sie tunaporwa ardhi yetu kila siku na kesi nyingi ni za kuporwa ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji, ndani ya migogoro hii ina siri kubwa bila kujua kiini chake ni wakati wa kufika kule na kupata ukweli zaidi” alielezea Adam Ole Mwarabu Kwa upande wake, Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli Nangiria ambaye anawakilisha watu hao asilia anaeleza kuwa, wao wamekuwa wakitambuana kwa desturi ikiwemo suala la ufugaji na maisha mengine, Jamii nyingine imekuwa wakiwaona wao ni watu wa tofauti kiasi cha kupora mali zao ikiwemo ardhi, mifugo na mambo mengine ya msingi. 
“Sie watu asilia tuna mahusiano mbalimbali na jamii zetu za kifugaji licha ya jamii zingine kutuingilia kwenye maeneo yetu na kupora ardhi yetu. Watu asilia tunahitajika kutambulika zaidi na hata kupatiwa huduma muhimu ikiwemo kujengewa shule, vyuo na mahitaji mengine ikiwemo haki na hutu kama watu wengine.” Alieleza Samweli Nangiria.

Kwa upande wake, .. ameweza kuipongeza tume ya Haki za Binadamu kwa kuweza kushughulikia suala hilo na hata kuandaa tukio hilo kwa kushirikisha wadau wengine wakiemo wao wa asilia.

“Tanzania ndio nchi ya kwanza kuaandaa kikao cha Afrika kwa watu hawa wa makundi maalum wa asilia, kilichofanyika mwaka uliopita. Hili ni jambo bora sana kwani watu asilia tunaendelea kutambulika zaidi.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa ya taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania, imeweza kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo suala la haki ya kuishi, Utawala bora na namna ya jamii hizo zinapotokea katika maeneo yao hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU