ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Mugabe amtosa Mnangangwa, asema kura yake anaipeleka upinzani

Monday, July 30, 2018


Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema hamuungi mkono mrithi wake Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa ndani ya chama tawala Zanu PF, kwa kile alichodai kuondolewa kwa nguvu madarakani na chama alichokianzisha.
 
Mzee Mugabe mwenye umri wa miaka 94, ametoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wake na wanahabari Jijini Harare,  ambapo taifa hilo la kusini mwa Afrika linafanya uchaguzi mkuu leo

Mugabe amesisitiza kuwa, hawezi kuwapigia kura watu waliomtesa na kwamba kura yake atampigia mmoja kati ya wagombea wengine 22 wanaowania nafasi ya urais.

"Namtakia kila kheri kiongozi wa chama cha upinzani cha Vuguvugu la Mageuzi ya Kidemokrasia, MDC, Nelson Chamisa katika uchaguzi wa leo . Kijana huyu ndio anaonekana kufanya vizuri na ndiye mgombea anayefaa", amesema Mugabe.

Zaidi ya raia milioni tano wa Zimbabwe wanajiandaa kumchagua Rais kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 38 bila Mugabe madarakani.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU