ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

House Boy Amchinja Mtoto Wa Bosi Wake Kisa Kumuomba Mua

Thursday, July 5, 2018

Jeshi la polisi mkoani Iringa, linamshikilia mfanyakazi wa ndani wa kiume, kwa tuhuma za kumchinja mtoto wa bosi wake kisa kuombwa kipande cha mua alichokuwa anakula mfanyakazi huyo.

Mtuhumiwa huyo, Gofrey Joshephat (29), mkazi wa Ipogolo, anadaiwa kumuua kwa panga mtoto huyo na kisha kuuweka mwili wake kwenye kiroba na kwenda kuutupa kwenye pagale jirani na nyumbani kwao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo jana Julai 4, saa nane mchana maeneo ya Kobwabwa B, Manispaa ya Iringa.

“Siku ya tukio mtuhumiwa alikuwa nyumbani na marehemu nyumbani akila muwa ambapo marehemu alimuomba mtuhumiwa kipande cha mua, alipokataa mtoto huyo alimtolea mtuhumiwa lugha ya kuudhi ndipo alipochukua panga na kuanza kumkata shingoni na mikononi na kuchukua kisu na kumchinja na kisha kwenda kumtupa kwenye pagale,” amesema.

Aidha, Kamanda Bwire amesema bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ikiwamo kumpeleka mtuhumiwa huyo kwa wataalamu kumpima kama ana akili timamu kiasi cha kumuua mtoto kisa kumuomba mua.

Mtoto huyo amezikwa jana katika makaburi ya familia huko Kibwabwa, Manispaa ya Iringa.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU