ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

BALAA LINGINE MCHANA HUU:.ADA ZA SHULE MUHULA MPYA PASUA KICHWA HII HAIJAWAHI KUTOKEA

Friday, January 6, 2017


NI pasua kichwa! Utaratibu mpya wa kulipa ada katika baadhi ya shule za binafsi nchini unaelekea kuwachanganya wazazi kutokana na ongezeko la kiwango cha malipo huku wamiliki wakidai kuwa hawana namna kwakuwa wanatimiza agizo la Serikali kuhusiana na vipindi vya muhula wa masomo 
Uchunguzi wa Nipashe uliohusisha mahojiano na wadau kadhaa wakiwamo wazazi na
wamiliki wa shule, umebaini kuwa agizo la Serikali la kuzitaka shule zote kuwa na mihula miwili ya masomo na siyo zaidi ya hapo ndilo linalotumika kama kigezo kwa baadhi ya shule kuwataka wazazi walipe ada za watoto wao kwa mikupuo miwili tu kwa mwaka ili kuendana na idadi ya sasa ya mihula kwa kipindi hicho; na siyo kama ilivyokuwa awali ambapo baadhi waliruhusu wazazi kulipa kwa mikupuo hadi minne kutokana na utaratibu waliokuwa nao wa mihula.
Matokeo yake, Nipashe imebaini kuwa baadhi ya wazazi wamejikuta katika wakati mgumu kwa sasa, sababu ikiwa ni kuwapo kwa ongezeko la hadi mara mbili ya kiwango cha fedha wanachotakiwa kuwalipia watoto wao.
Hata hivyo, uchunguzi wa Nipashe umebaini vilevile kuwa baadhi ya shule zimelazimika kuwasikiliza wazazi kwa kuruhusu waendelee kulipa kwa mikupuo zaidi ya mwili, lengo likiwa ni kuwapa fursa ya kuzoea utaratibu huo mpya unaoendana na idadi ya mihula.
Nipashe ilibaini kuwa katika baadhi ya shule ambazo ada yake ni Sh. milioni tatu kwa mwaka, ulipaji wa mikupuo minne ulikuwa Sh. 750,000 kwa muhula, lakini sasa kutakuwa na malipo ya mikupuo miwili ambayo mzazi atalazimika kulipa Sh. 1,500,000 kwa muhula.
Aidha, kwa shule ambayo ada yake ni Sh. milioni mbili kwa mwaka, ulipaji wa mikupuo minne ya zamani ulikuwa Sh. 500,000 kwa muhula, lakini kwa mihula miwili ya sasa, mzazi hulazimika kulipa Sh. milioni moja kila muhula. 
Baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, pamoja na mambo mengine, Prof. Joyce Ndalichako, alitangaza uamuzi wa Serikali wa kupiga marufuku utaratibu wa baadhi ya shule wa kuwa na mihula zaidi ya miwili kwa mwaka mmoja wa masomo.
Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, baadhi ya wazazi wenye watoto wanaosoma shule za msingi binafsi walisema utaratibu wa sasa unawapa wakati mgumu kwa sababu hali ya kifedha imekuwa ngumu na zaidi ya yote, walishajiandaa kitambo kuwalipia ada watoto wao kwa utataribu wa awali wenye mikupuo zaidi ya miwili.
“Mimi nina watoto watatu, na kwa wastani kila mtoto huwa namlipia ada ya Sh. 500,000 kwa kila mkupuo katika awamu tatu kwa mwaka… sasa naambiwa nilipe Sh. 750,000 kwa kila mtoto kwa sababu ni lazima nimalize kwa awamu mbili, nitaziotoa wapi? Sikuwa nimejiandaa kwa mabadiliko hayo,” alisema mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Mama Halima, mkazi wa Kijitonyama. 
Magreth Mshana, mmoja wa wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule binafsi iliyopo jijini Dar es Salam, alisema ada kulipwa katika mihula miwili inawezekana, lakini kuna changamoto ya wamiliki wa shule hizo kupandisha ada kiholela bila kujali ubora wa huduma inayotolewa na shule husika na hivyo ni bora Serikali ikaingilia kati kwa kutoa ada elekezi kama inavyofanya katika kusimamia mafuta na nishati.
WAMILIKI WA SHULE
Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Vyuo na Shule Binafsi Tanzania (Tamongsco), Benjamin Nkonya, alisema ulipaji wa ada katika shule hizo kwa awamu mbili umetokana na utekelezaji wa tamko la serikali na hivyo wazazi na walezi wa wanafunzi hawana namna nyingine isipokuwa ni kujipanga upya kwa utekelezaji.
Alisema njia mojawapo ya kufanikisha jambo hilo ili hatimaye watoto wao waendelee kupata elimu bora ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Alisema katika serikali ya sasa ya awamu ya tano, wazazi wanatakiwa kufuata na kuunga mkono kauli ya kubana matumizi kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia fedha katika matumizi yasiyo ya lazima na badala yake waelekeze nguvu katika shughuli za maendeleo ikiwamo elimu ya watoto wao.
“Wazazi, walezi wapunguze starehe. Michango isiyo ya lazima kama harusi, mtu anachangia hadi laki (Sh. 100,000) au milioni kufanikisha tukio la siku moja tu, hapo hapo ukimwambia ada ilipwe kwa awamu mbili, anaona mzigo. Ukweli ni kwamba wabane matumizi, waache kushinda baa,” alisema Nkonya.
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Lord Baden Powell iliyopo Bagamoyo, Kanali Mstaafu Idd Kipingu, alisema ada kwa mwaka shuleni kwake inalipwa kwa awamu mbili, ingawa wametoa fursa kwa mzazi au mlezi anayeshindwa kulipa kwa awamu hizo mbili, kulipa mara tatu.
“Inalipwa kwa awamu mbili, lakini mzazi akijieleza na kutokana na ugumu wa fedha katika kipindi cha Januari, atalipa kwa awamu tatu,” alisema Kipingu.
Agustino Mwalongo, mmoja wa viongozi wa Shule ya Sekondari Barbro iliyopo jijini Dar es Salaam, alisema ada kwa mwaka kwao hulipwa kwa awamu mbili kulingana na mwongozo wa serikali wa kuzitaka shule kuwa na mihula miwili tu kwa mwaka.
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Winning Spirit iliyopo mkoani Arusha, Maximillian Iranke, alisema ada katika shule yao inalipwa kwa awamu nne, ingawa mihula ya masomo ipo miwili kulingana na mwongozo wa serikali.
“Ada inalipwa kwa awamu nne, Januari, Aprili, Julai na Septemba… lakini mihula ya masomo ni miwili kama serikali inavyosema,” alisema Iranke.
MSISITIZO WA AGIZO LA SERIKALI
Mwanzoni mwa mwezi uliopita, Kaimu Kamishna wa Elimu, Venance Manori, alisema wizara hiyo itazifutia usajili shule zote binafsi zitakazobainika kukiuka agizo hilo la kuzitaka kuwa na mihula miwili ya masomo kwa mwaka badala ya mitatu hadi minen kwa baadhi yao.
Ili kutekeleza azma hiyo, Manori alisema wizara hiyo iliwaagiza wakaguzi wa shule pamoja na maofisa elimu wa wilaya, kufanya ukaguzi katika shule binafsi zilizoko katika maeneo yao; kubaini kama kuna shule binafsi zilizokaidi kutekeleza Waraka wa Elimu Namba Moja wa Mwaka 2015.
Alisema wizara yake ilitoa waraka huo ikiwa ni njia ya kukazia Waraka wa Serikali Na. 5 wa Mwaka 2012 ambao ulikuwa unaelekeza mihula ya masomo kwa shule za sekondari na vyuo vya ualimu, ifanane ili kuepusha usumbufu kwa walimu na wanafunzi.
Waraka huo ulifafanua kuwa kila muhula utakuwa na likizo fupi na likizo ya mwisho wa muhula na siku za masomo kwa mwaka zitakuwa ni 194.
Pia waraka huo unataka siku za michezo ya Umitashumita na Umiseta kwa shule za msingi na sekondari, zifanane kwa shule zote.
“Ule waraka ulisambazwa kwa mamlaka zote za utekelezaji ukiwamo umoja wa shule binafsi na taasisi inayosimamia shule za dini ya Kikristo na ile ya shule za Kiislamu, hivyo hakuna kisingizio cha mtu kutopata huo waraka… lazima wautekeleze,” alieleza Manori. 

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU