ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

POLISI YASHIKILIA WATANO KWA KUNAJISI NA KUUA MTOTO-ARUSHA Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ

Thursday, June 23, 2016


POLISI mkoani hapa inawashikilia watu watano kwa tuhuma za kumuua mtoto wa miaka minne baada ya kumnajisi na kumvunja shingo Jumatatu iliyopita. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuf Ilembo, alisema wanawashikilia watu hao ambao majina yao hakuyataja na upepelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani. Ilembo alisema tukio hilo lilitokea Juni 20, saa 3:30 usiku kwenye makaburi ya Baniani yaliyoko Kata ya Unga Limited, jijini hapa. Alisema baadhi ya watu waliuona mwili wa mtoto huyo ukiwa umetupwa kandokando ya njia ya watembea kwa miguu, karibu na mfereji wa maji umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwao. Alidai kabla ya kufanyiwa vitendo hivyo, mtoto huyo alikuwa akicheza na wenzake nje kidogo ya nyumbani kwao na ilipofika majira ya saa 12:00 jioni, kwa mujibu wa marafiki zake, alifika mtu mmoja mwanamume. Walidai kuwa mwanamume huyo alikuwa mrefu na alivaa suruali na kumwambia mtoto huyo amfuate akamnunulie pipi na ndipo alipomfuata na hakurudi tena. walisema ilipofika majira ya saa 1:30 usiku baada ya wazazi kuona mtoto wao amechelewa kurudi nyumbani, ikiwa si kawaida yake kuchelewa, walianza kumtafuta kwa kuwaarifu majirani pamoja na kutoa taarifa katika Msikiti wa Esso. Mmoja wa majirani hao alisema baadaye kidogo walipokea taarifa za mtoto kuonekana katika njia ya watembea kwa miguu katika makaburi ya Baniani akiwa amekufa, ndipo walipotoa taarifa kituo cha Polisi Wilaya ya Arusha Mjini. Alisema polisi waliuchukua mwili wa mtoto huo na kuupeleka Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Mount Meru, kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa daktari na ilibainika alinajisiwa na kuvunjwa shingo, hivyo kusababisha kifo chake.


No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU