ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

WAZIRI MKUU MSTAAFU LOWASSA WALIVYOKIMBIANA NA MFUASI WAKE WA KARIBU SANA BUNGENI JANA SOMA HAPA LIVE!!

Wednesday, November 2, 2016


MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba, jana alikwepa kusalimiana na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa mjini Dodoma. Lowassa ambaye alikuwa ameandamana na Waziri Mkuu mstaafu, Fredereck Sumaye na viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walitembelea bungeni kwa mwaliko wa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe. 
 
Vigogo hao ambao walitambulishwa na Mwenyekiti wa Bunge, Najma Murtaza Giga waliamsha shangwe kwa wabunge wa kambi ya upinzani, huku wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa wamekaa kimya na wengine wakitabasamu. 
Baada ya Bunge kuahirishwa mchana, viongozi hao walitoka nje na kusalimiwa na wabunge mbalimbali, akiwemo Mbunge wa Newala, George Mkuchika, Mussa Ntimizi (Igalula), Venance Mwamoto (Kilolo) ambao wote wanatoka CCM. 
Serukamba ni moja ya vijana watiifu kwa Lowassa, ambaye kwa miaka kadhaa, alikuwa akimuunga mkono na wakati wote wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM katika kinyang’anyiro cha kuwania urais mwaka 2015 alikua mstari wa mbele. 
 
Taarifa zilizojiri katika mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa, sababu iliyomfanya Serukamba amkimbie Lowassa ni kuogopa taarifa kumfikia Rais Dk. John Magufuli, ambapo wanaCCM waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa ndani ya chama hicho hawaaminiki katika Serikali ya awamu ya tano. 
Katika msafara huo, Lowassa na Sumaye walikuwa wameandamana na wajumbe wenzao wa Kamati Kuu ya Chadema ambao ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Profesa Abdallah Safari na waziri wa zamani wa Serikali za awamu ya pili na tatu, Arcado Ntagazwa.


Chanzo-Mtanzania

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU