ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Meli yenye bendera ya Tanzania yanaswa Ugiriki ikipeleka vilipuzi Libya

Thursday, January 11, 2018

Tanzania imefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.
Maafisa wa Ugiriki wanaoshika doria baharini wamesema wanaizuilia meli iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania ambayo ilikuwa imebeba vilipuzi.
Meli hiyo inadaiwa kusafirisha vilipuzi hivyo kutoka Uturuki kwenda
Libya, kinyume na marufuku iliyowekwa ya kutosafirisha silaha kwenda Libya.
Maafisa wanasema meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa vilipuzi pamoja na kemikali zinazotumiwa kuunda vilipuzi ikiwemo.
"Maafisa wa kushika doria baharini wamezima bomu lililokuwa linasafiri," afisa mkuu wa walinzi hao wa Ugiriki Yiannis Sotiriou aliwaambia wanahabari, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ANA.
Wizara ya Safari za Baharini ilisema meli hiyo ilisimamishwa ikiwa katika kisiwa cha Crete kusini mwa Ugiriki wikendi baada ya maafisa kupashwa habari na mdokezi.
Ilisindikizwa hadi katika bandari moja kisiwa hicho cha Crete na kufanyiwa ukaguzi.
Crete
Sotiriou alisema meli hiyo ambayo ilinaswa Jumamosi ilikuwa pia na kasoro nyingi na haikufaa kuwa baharini.
"Ingesababisha madhara makubwa sana kwa watu na mazingira pia," amenukuliwa na AFP.
Nahodha wa meli hiyo kwa jina Andromeda alidai ilikuwa inasafiri kuelekea Djibouti lakini baadaye ikabainika kwamba ilikuwa inasafiri kuelekea mji wa bandarini wa Misrata nchini Libya.
Shirika la AFP linasema mabaharia hao wanane waliokuwa kwenye meli hiyo watafikishwa mbele ya mwendesha mashtaka leo.
Watano kati ya mabaharia hao ni raia wa India, wawili wa Ukraine na mmoja wa Albania.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU