
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule hiyo inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko la
Ardhi lililotokea mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama wakati Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa maeneo ya Ihungo Sekondari Mkoani Kagera hawapo pichani mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari Ihungo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakitoka kwenye ukaguzi wa shule ya Sekondari Omumwani mkoani Kagera. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment