Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kinga ya mwili ni kitu gani na je ni nini tufanye ili kuiongeza hiyo kinga ndani ya miili yetu. Suala la kuimarisha na kuiongeza kinga ya mwili linapaswa kuwa ni jambo endelevu la kila siku.
Hakuna dawa au chakula cha kula siku moja na kuponya tatizo la kushuka kinga ya mwili milele. Kinga ya mwili huongezeka ama kupungua kila siku kutegemea na umekula nini, umekunywa nini au hali ya ubongo wako kwa ujumla ipoje kwa siku hiyo, mathalani kama umeshinda una hasira hasira tu kutwa nzima lazima na kinga yako itapungua.
Mwili ulibuniwa na Mungu uweze kujitibu wenyewe bila kuhitaji DAWA YOYOTE. Ulivyo ni vile unavyokula na kunywa.
Shida ni kuwa watu wengi hatujui tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe na wengine tunakula kwa kuongozwa na tamaa tu, hatuli chakula kwa mwongozo
Fanya chakula kiwe ndiyo dawa zako na dawa zako ziwe ni chakula unachokula. Kinga yako inapokuwa na nguvu ya kutosha huwezi kuugua ugonjwa wowote kirahisirahisi.
Vifuatavyo ni vyakula 14 vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako:
1. MTINDI (yoghurt)
Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na