Dar es Salaam. Wakati zikiwa zimebaki siku nane kufikia Oktoba Mosi ambayo imetangazwa kuwa siku ya kupanda miti, Shirika la
Kimataifa la Kutetea Haki za Wazee (HelpAge International) limekumbushia kuwa siku hiyo pia huadhimishwa kama siku ya wazee duniani.
Meneja miradi wa shirika hilo, Joseph Mbasha amesema kuwa kitaifa mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyika Mbarali mkoani Mbeya kwa upande wa Tanzania bara na kwa Zanzibar yatafanyika visiwani Pemba.
Mbasha amesema maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo hufanywa Oktoba Mosi kila mwaka kote duniani yanalenga kutambua mchango wa wazee na kwamba siku hiyo ni muhimu kwao.
Amesema katika maadhimisho ya mwaka huu wataangazia mambo mbalimbali hasa changamoto zinazowakabili wazee nchini.
No comments:
Post a Comment